KaziIendelee
JF-Expert Member
- Oct 30, 2013
- 327
- 229
Badilisha lugha kiingereza wengine tunajua yes na no, ze maza, ze faza, zego, ze kamu.
Msaada mkuu,swali lipo hivyohivyo
Ndugu wanaJF naombeni tafsiri ya swali hii na mniambie linahitaji nini,
"It suffices to argue that the era of industrial revolution in Europe especially Britain was a prosperous one the working class".Critically assess this statement.
Kuna shida kwenye grammar ya swali,. Angalia vizuri uliandike vizuri Hasa hapo kwenye maneno "prospectus one the working class"
Kuna shida hapo,
Its either kuna neno limekosewa, ama kuna neno halipo.
Mfano lingeweza kuwa "prospectus one AMONG/ To the working class"
Au
"PROSPEROUS one TO the working class"
Vinginevyo hivyo lilivyo halileti maana.
Comrade,
nadhani sasa nimejua kuwa kuna tatizo kubwa katika mfumo wa elimu wa Nchi yetu.mada ndogo inawachanganya watu hata wenye degree zao! tazama dissemination inayo fanywa na baadhi ya wachangiaji wanadiriki kusema neno prosperous limekosewa kwa hiyo lilitakiwa kuwa prospectus kwasababu yeye ndio analo lijua!! ukishangaa ya MLUGO UTAONA YA WATUMA SALAMU WA JF!!
Ama kuhusu swali lako, liko sahihi na muulizaji bila shaka ni mwalimu anataka kupima mambo kadhaa.pamoja na hoja ya msingi mwalimu anataka kuona ni kwa jinsi gani mwanafunzi anaweza kujenga hoja zenye kushawishi kuwa mapinduzi ya viwanda hususan Uingereza kwamba yalichangia mabadiliko makubwa ya kipato cha wafanyakazi"working class".PROSPEROUS maana yake ni kufanikiwa hasa kwa kipato.
Na wewe mleta mada hivi unawezaje kuleta swali kama hili hapa wakati unajua humu kuna watuma salamu wengi na wapiga debe kuliko watu makini? Wakati mwingine jaribu kukaa na wenzako darasani tafuteni majibu hasa Answers.com na kwingineko au tuma kwa JERUSALEMU QUICK ANSWERS.COM
Ok kama ni prosperous one among the working class, sasa twende pamoja;
1. Tuliewe sawali,
Namna nzuri zaidi na rahisi ya kulielewa swali nadhani nikwanza kulitafsiri kwa lugha inayo eleweka zaidi - kiswahili.
Kwakiswahili swali lingesomeka
"yatosha kusema kuwa kipindi cha mapinduzi ya viwanda ulaya na hasa uingereza kilikua kipindi cha mafanikio miongoni mwa tabaka la wafanya kazi. Chambua tamko hili kwaundani.
2. Academic meaning ya swali.
Katika mazingira ya shule unapokutana na swali linalokutaka ku assess,discuss or critically analyze. Na maneno hayo kuwekwa mwisho wa swali, basi tambua utatakiwa kutoa maelezo yenye pande mbili, yaani Arguments FOR and AGAINST the statement.
3. Tujibu swali sasa
Katika swali tulilonalo utatakiwa kutoa points kwanza zinazo support statement ya swali, yaani points zinazo onyesha kuwa tabaka la wafanyakazi lilifaidika sana na kipindi hicho cha mapinduzi ya viwanda ulaya na Hass uingereza. Halafu Kisha utatoa point zinazo onyesha kuwa pamoja na kua kipindi cha mafanikio kwao kilikuwa na changamoto flani, sasa unaeleza changamoto za kipindi hicho kwa tabaka hili la wafanya kazi.
Comrade, natumai nimesaidia.
Asante mkuu