Kinzudi ni eneo lililopo nyuma ya baraza la mitihani. Eneo lenye hizi plots ni karibu na shule ya Rightway. Eneo lipo kati ya shule ya Rightway na TATEDO, kama wewe ni mwenyeji kidogo unaweza kupafahamu.
Eneo linaweza kufikika kwa njia kama tatu hivi:
1. Ukipanda na njia ya kuelekea Goba tokea Samaki Wabichi, unachepuka kwenye njia panda ya kuelekea TATEDO.
2. Ukitokea Morogoro, unachepuka Mbezi Mwisho kuelekea Goba Kijijini, unaendelea na njia kama unaelekea Samaki lakini unachepuka Tanki la maji lililopo kushoto kabla ya kufika kanisani.
3. Unaweza pia ukatumia njia panda ya Africana kuelekea Salasala, unapanda mpaka kwenye eneo linapopita bomba la Song gas ulizia shule ya Rightway.
4. Kwa daladala unaweza kupanda daladala za Tegeta unashuka Mbuyuni unapanda daladala za Kinzudi kupitia Mboma road unashuka mwisho ulizia kwa Kajanja, utakuwa umefika.