Plug Vs fuel consumption

Plug Vs fuel consumption

Baringongo

Member
Joined
Dec 12, 2016
Posts
97
Reaction score
90
Habari za jumapili.

Ninatamani zaidi kufahamu kama upo uhusiano wa Moja Kwa moja kati ya kuongezeka Kwa utumiaji wa mafuta (petroleum) katika gari na muda uliotumia plug.

Pia muda sahihi wa kubadilisha plug Yani kama Kuna kilometers specific zikifika utahitaji kuchange plugs.

1651925394370.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za jumapili.
Ninatamani zaidi kufahamu kama upo uhusiano wa Moja Kwa moja kati ya kuongezeka Kwa utumiaji wa mafuta (petroleum) katika gari na muda uliotumia plug.
Pia muda sahihi wa kubadilisha plug Yani kama Kuna kilometers specific zikifika utahitaji kuchange plugs. View attachment 2257952

Sent using Jamii Forums mobile app
Uhusiano upo tena uhusiano wa karibu.

Muda wa kubadili plug itategemea na plug ulizofunga kama ni original au hizi za bei rahisi.
 
Endelea tafadhari

Spark Plug ndio zinachoma mafuta kwenye engine.

Zikiwa hazichomi vizuri nguvu itazalishwa ndogo, Engine Control unit itaamuru mafuta yaongezwe ili izalishwe nguvu nguvu nyingi zaidi ili kucompesate nguvu iliyopotea. Na hapo ndio ulaji wa mafuta utauona wazi.

Zikiwa na moto mkali kuliko kawaida, Joto litakuwa kali sana kwenye engine, kutatokea pre-ignition (yaani hilo joto litapelekea mafuta yaungue kabla spark plug haijatema cheche). Bado nguvu itakuwa ndogo sababu mafuta hayaungui kwa wakati, itaamuliwa mafuta yaende mengi.

Lakini hili la plug kuwa na moto mkali ni baya zaidi sababu linaharibu parts za engine yako.
 
Back
Top Bottom