Plywood kama fulsa mpya kwa wakulima wa Miti.

pelezicr

Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
28
Reaction score
17
Ni jambo la faraja sana kwa mkulima wa MITI kusikia kuwa miti ya mikaratusi/milingoti inahitajika kwa ajili ya kutengenezea plywood. Uhitaji wa mti wa mkaratusi ni mkubwa sana kwa sasa katika viwanda Gina kwa ajili ya kutengenezea plywood. Wilayani Mufindi/Mafinga tayari kuna viwanda vinavyochakata mikaratusi ili kutengeneza plywood.

Miti ya mikaratusi yenye umri unaoanzia miaka mitano humenywa katika mashine maalumu na kutoa veneer ambazo huunganishwa katika kutengeneza plywood. Inaelezwa kuwa bado upo uhitaji mkubwa wa plywood duniani. Hii inatuhakikishia uhitaji mkubwa wa mikaratusi/milingoti kama raw material katika viwanda hivi.

Jambo la msingi ni kuzalisha miti yenye ubora wa hali ya juu utakaowezesha miti kununulika.

Plywood is a material manufactured from thin layers or "plies" of wood veneer that are glued together with adjacent layers having their wood grain rotated up to 90 degrees to one another. It is an engineered wood from the family of manufactured boards which includes medium-density fibreboard and particle board. Wikipedia
Did you know: In the simplest case of three-ply sheets, the back veneer is laid flat and is run through a glue spreader, which applies a layer of glue to the upper surface. encyclopedia.com


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • 153130176468727209120646b719e605007985522fd40c30e13b823e97d8b4e144fecfafc2503cadcd999c449de26...jpeg
    140.4 KB · Views: 28
  • images%20(5).jpeg
    9.6 KB · Views: 33
Mada kama hii huwezi kupata wachangiaji. Ni mpaka uandike " Hatimaye Wema karudiana na Diamond ".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba picha ya mikaratusi mimi miti naijua kwa majina ya kienyeji
 
Mikaratusi ni mizuri lakini inakausha sana vyanzo vya maji na inatumia maji mengi sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi hii miti siwezi kuipanda hata kidogo maji ni uhai

Sent using Jamii Forums mobile app
hiyo miti ya Mikaratusi(Eucalyptus) inahitaji maji mengi sana ili kukua

Lakini pia ni aina ya miti ambayo hukua kwa haraka sana,yaani ndani ya miaka 6 unaweza kuanza kuvuna poles.

Pia miti hii ina sifa moja ya kipekee,baada ya kufanya clear feeling,visiki vyake vinaweza kuchipua tena na ukavuna poles tena na tena,kitendo hiki huitwa Coppies
 
Naomba picha ya mikaratusi mimi miti naijua kwa majina ya kienyeji

Hope utaufahamu vizuri sasa.

Ni mti unaostawi maeneo mengi ya hapa Tanzania.
 

Attachments

  • eucalyptus-grandis-trees.jpg
    80.8 KB · Views: 19

Ni kweli kabisa mdau, ila kwa hili la kusema miti ya Mikaratusi kuwa anahitaji maji mengi sana naomba nipingane nawe, kwa uzoefu wangu na tafiti zinaonyesha kuwa muhindi unaweza kuwa na uwiano mkubwa zaidi kuliko mti wa mkaratusi.

Kwa nyongeza ni kwamba kuna aina zaidi ya 2000 za Mikaratusi Duniani na kwa Tanzania zipo zaidi ya 40 ambazo zinatofautiana sana kwa kila kitu kuanzia ukuaji, mazingira na pia mazao yake.
 
Mimi hii miti siwezi kuipanda hata kidogo maji ni uhai

Sent using Jamii Forums mobile app

Unaweza ukawa sahihi ingawa ukija kuangalia upande wa pili ni kwamba wanadamu wanahitaji malighafi pia hasa mbao.

Na hapa duniani ni mti mmoja tu ambao unasifa nyingi zaidi za ukuaji wa haraka, kutoa mazao mengi na mti unaoweza kustahimili mazingira tofauti na mti huo ni Mkaratusi.

Na kwa namna nyingine huwezi ukasema unapenda maji ukauacha mti unaoweza kusaidia duania kuhifadhi mazingira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…