Manka, pitia hili jukwaa MziziMkavu kadadavua uzuri.
Kwa ufupi sickle cell inatokana na viasili (genes), ambazo hurithiwa. Inahitaji pair ya viasili hivi ili ugonjwa udhihirike, ama sivyo unaweza kuwa na weak gene na isijitokeze japo inaweza kujitokeza kwa watoto.
Ugumu wa kuwa na maisha marefu ukiwa na sickle cell ni kuwa kwanza inasababisha upungufu wa damu mwilini(sickle cell anaemia) kwa sababu ya ku-impair uzalishwaji wa chembe nyekundu za damu. Chembe hizi pia ndo husafirisha oxygen, mahitaji ya mtu mzima ni tofauti na ya mtoto.