Ngahekapahi naona umefika mbali saana....Pneumonia ni ugonjwa unaowapata both watoto na watu wazima, sina hakika unaongelea kwa group gani sasa, maana baadhi ya dalili zaweza tofautiana.
Naomba niongelee kwa watoto (mimi ni mdau mkubwa wa afya za watoto). Pneumonia kwa watoto ni ugonjwa simple sana (lakini unaongoza kwa kuua) ambao wala hauhitaji ujuzi mwingi na test sophisticated kuugundua na kutoa matibabu husika. Dalili kubwa kwa watoto ni kikohozi, na/au mafua, na/au homa, na kupumua kwa shida na/au haraka. Daktari atamchunguza kwa kuhesabu idadi yake ya pumzi kwa dakika, kama imevuka kiwango cha kawaida basi ni Pneumonia. Daktari pia anaweza msikiliza mtoto kifua kwa stethoscope na kusikia crepitations.
Udharura wa Pneumonia unakuja kama ni Pneumonia kali (kuna vigezo vya kusema hivyo)...mara nyingi hakuna first aid unayoweza kutoa nyumbani zaidi ya kumuwaisha mtoto hospitali akapate huduma husika. Pneumonia sasa hivi inaua watoto wengi zaidi hata ya Malaria.
NB:
Sputum Culture ni kipimo ambacho unatoa makohozi ili kutambua ni vijidudu gani (microbacteria) wamesababisha hiyo Pneumonia, mara nyingi hufanyika kwa Pneumonia Sugu na/au Tuberculosis.
Pleural Effusion ni complication ya Pneumonia pale inapoendelea kiasi cha mapafu kujaa maji kwenye pleural cavity...hii ni complication late sana ya Pneumonia sugu au Tuberculosis, na hayo maji maji yanaweza kutolewa kwa sindano ili kupima kujua ni vijidudu gani vinasababisha.