Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Kipato cha walio wengi ni mshahara, hata kama unafanya biashara ni muhimu kujiwekea mshahara wako, hii itakusidia kuiheshimu faida na kutokuigusa.
Matumizi ya muhimu katika mshahara ni chakula, kodi ya nyumba na usafiri. Haya yanatakiwa kutolewa katika mshahara kabla hujapanga mipango yeyote mingine.
Matumizi yanayofuatia ni
1. Mipango ya muda mrefu, hii ni pesa itakayokusaidia uzeeni kama utajaliwa kuishi kufikia uzee. Hakuna kitu kibaya kama uzee bila pesa. Kumbuka katika umri huu huna nguvu za kufanya kazi. Licha ya kuwa mwanachama wa mifuko ya jamii ikiwezekana kuwa na pensions fund yako binafsi. Ukianza kuweka laki moja kila mwezi ukiwa na miaka 25 mpaka ukifikisha miaka 50 unakuwa umeuaga umasikini.
2. Mipango ya muda wa kati hii inakuwa na ki pochi cha pili. Katka mipango hii unaweza kupata pesa za kununua kiwanja na kujenga makazi. Hatimae unapunguza uzito katka matumizi ya mshahara. Hapa ikiwezekana uwekezaji uwe mkubwa kuliko poxhi ya awali.
3. Kifuko cha mwisho ni mipango ya muda mfupi. Hapa unaweka manununzi ya nguo na pesa ya kwenda likizo. Mipango ni muhimu, usinunue nguo kwakua bei imepungua, kama haiko kwenye mipango yako achana nayo.
Ukiwa na nidhamu hii unaweza kuitwa bahili kwani hata pesa ya kumwagilia moyo ni lazima iwe kwenye mipango. Kuna wakati hata muda wa kumwagilia moyo utawaza kuongeza chochote kwenye vifuko vyako.
Kinacho angusha wengi ni huduma za Jamii. Kama serikali haijawekeza ipasavyo katika huduma madhlani za afya, mtu wako wa karibu akiugua mfano saratani, gharama za kwenda Ocean Road kwenye mionzi na huduma za kila siku zinaweza kumaliza akiba yako yote.