POINTS 10 ZA UJENZI : UDONGO MFINYANZI NA UJENZI

POINTS 10 ZA UJENZI : UDONGO MFINYANZI NA UJENZI

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
MAKALA YA 6
Karibuni tena katika Makala ya ujenzi. Leo tujifunze machache juu ya Udongo wa Mfinyanzi na Uhusiano wake katika Ujenzi

1.Mfinyanzi ni moja kati aina kuu tatu za udongo.
-sifa aa Mfinyanzi
  • Una Tanuka ukiwa na maji na kusinyaa ukikauka
  • Una tunza maji(siyo rahisi maji kupenya)
  • Una shika mana.
2.Njia nyepesi za kujua kama udongo wako ni Mfinyanzi.
A.​
-Chukua udongo wa kujaa kiganya​
-Ulowanishe maji kidogo​
-Tengeneza umbo la mpira (duara)​
-Ukiona huo mpira umeshikamana bila hata kumong'onyoka ujue huo ni mfinyanzi​
B.​
-Chukua udongo kidogo​
-ulowanishe maji​
-Fikicha huo udongo kwenye vidole vyako​
-Ukiona una nata nata ,basi huo ni mfinyanzi​
C.​
-Kama umefika kwenye eneo lako kipindi cha kiangazi,​
-Ukaona kuna nyufa kwenye ardhi,ambapo hata kijiti kinapenya huo ni mfinyanzi​

2.maeneo yenye udongo wa Mfinyanzi yapo ya aina mbili.
Maeneo yenye mfinyanzi mkali.
-udongo unakuwa una kiwango kikubwa cha Mfinyanzi.mfano
  • Mbezi Juu na Makongo juu -wilaya ya Kinondoni
  • MbeziLuis,Kimara,Goba,Kibamba,Kiluvya,Msigati -wilaya ya Ubungo
  • Kinyerezi,Segerea - wilaya Ilaya
maeneo yenye mfinyazi tulivyo,hapa udongo una kiwango wastani cha mfinyanzi. Mfano
  • Pugu Kajiungeni,Majohe,Buyuni,Msongola-Wilaya ya Ilala
  • Bunju B ,Mabwe Pande - Wilaya ya Kinondoni.
  • Chamazi,Mgeni Nani -wilaya ya Temeke
3.Faida za Udongo wa Mfinyanzi ni.
-Haumong'onyoki, hii ni kutokana na sifa ya punje sake kushikamana sana.

-Unazuia usambaaji wa mizizi ya miti karibu na jengo lako.

-Unatunza maji kwa mda mrefu,hii ni kutokana na sifa ya kutoruhusu maji kupenya

4.Hasara za Udongo wa mfinyanzi
-Ni ngumu kuchimba msingi au Shimo,kwahiyo mtu huingia gharama kubwa na mda mrefu kwenye kuchimba .
-Ngumu kuotesha mimea
-Haupo stable/imara kwenye kubeba msingi,hii ni kwakuwa unatanuka na kusinyaa.

5.Athari kubwa ya Ujenzi katika Udongo huu ni
Nyufa kwenye msingi na kuta
-Udongo karibia na msingi unapolowa maji kipindi cha mvua ,unatanuka
-Kuna upande Unatanuka sana kwenye kidogo.na kukandamiza msingi au kusukuma juu.
-kiangazi kikija,utasinyaa kwa viwango tofauti.
-Mabadiliko hayo hupelekea msingi kuvunja taratibu na kuweka nyufa au
-Kusukuma juu sehem ya jengo.

6.Athari nyinginee
Milango na madirisha kuwa migumu kufunga na kufungua
-sehemu moja ya jengo ipo juu,nyingine chino
Uwazi kuzunguka madirisha na Milango
 
7.Kudhibiti Athari za mfinyanzi.
(Udhibiti kabla Ujenzi)
A.Utumizi wa Kemikali,
-Hapa unatumikia Quicklime au Ordinary Portland Cement/Simenti za ujenzi hizi,iwe nyeupe au ya Kijivu.
-Changanya Udongo uliopo kwenye ardhi ya shimo lako la msingi na simenti
-Mwagia maji ya kutosha,yale maji yatasaidia kueneza simenti chini kina kama cha sentimita 15

B.Utumizi wa Mchanga
-Mwaga mchanga kimo cha sentimita 5 kuzunguka eneo lote la msingi

(Udhibiti kipindi cha Ujenzi )

8.Udhibiti
C.Zege lenye nondo kwenye msingi.
-Kitako cha msingi kijengwe kwa Zege lenye nondo.itasaidia kuimarisha msingi.
-Pia kwenye level ya juu ya msingi msingi(Plinth) mkanda wake uwe na zege lenye nondo.
-Nondo kwenye boksi moja la hiyo kitako na Mkanda ziwe nne,,na si chini ya hapo
-
D.Utumizi wa Mchanga
-Kuta za msingi wako zote kutoka chini hadi juu,zizungukwe na mchanga

9.Udhibiti
(Baada ya Ujenzi)
E.Dhibiti mzunguko wa maji karibu na msingi.
-maji ya bati yakusanywe na Gutter
-downpipe isimwage maji kwenye ardhi ya msingi
-Zungusha kibaraza kwenye kuta zako.
-Usiruhusu weka mfumo wa kukusanya maji ya mvua kwenye eneo.

10.Ushauri
Unapotaka kujenga kwenye maeneo ya mfinyanzi,Ubahiri weka pembeni.
Kwani huu udongo una haribu jengo kwa kuweka manyufa makubwa.
-Ni ngumu na gharama sana kurekebisha nyumba zilizo na nyufa.
-Tafuta mtaalam akusaidie
Nakaribisha maswali na maoni

Mwezi wa 4,nitakuwa likizo,wale watakao hitaji msaada wa kukagua viwanja vyao na Majengo yao, kuwa huru kunitafuta.
-Huduma itakuwa ya bure ,Uta gharamia nauli tu.
 
images-38.jpeg

Ardhi ya mfinyanzi
 
Back
Top Bottom