Poland yamvimbia Russia, huu ujasiri wanautoa wapi?

Article 4 ndiyo inaenda kuanzisha mazungumzo ya kuingia article 5.

Sasa unataka watu waanze kupigana vita bila kujadiliana?
 
Wazungu wanapenda kuuwana sana bora nilivo zaliwa mwafrika
 
Reactions: Lax
Kama zimeingia kwenye anga lake ni haki yake kufanya hivyo... Kinachonishangaza ni Poland kutoiadhibu Urusi kwa kukiuka anga lake

Kutoiadhibu vipi wakati wamezidungua? Ndo adhabu ipo hapo. Imenishangaza hadi Poland ana mdindia Mrussi? Mrusi anaanza ku fail sana.
 
Duh Poland hii hii ambayo chini ya miezi miwili ilinyanyua mikono juu dhidi ya wasoviet?
 
Hivi huko Bongo elimiyenu ikoje? Eti Poland kutungua drone za Kirusi ni kumdindia Russia!
Si Poland tu hizo drone hata zingepita Bongo Bado zingetunguliwa
 
Duh Poland hii hii ambayo chini ya miezi miwili ilinyanyua mikono juu dhidi ya wasoviet?
Umesoma nilichoandika kweli mkuu.

Kwanini unasema Poland ilinyanyua mikono miezi miwili dhidi ya Wasovieti. Mbona huwataji Nazi Germany?

Kwenye ile vita nani alianza uvamizi wa Poland kati ya Soviet Unioni na Nazi Germany.

Ni sawa na Soviets walipovamiwa na Nazi Germany, alafu muda huohuo Japan iivamie USSR. Hao USSR wasingeshinda hata Marekani ingemwaga misaada kiasi gani.
 
Kwani Russia ana nini cha maana?

Ukrain kaishindwa leo miaka lukuki
Mkuu nawaza msaada anaoupata Ukraine dhidi ya Urusi angeupata Palestina dhidi ya Israel hivi hali ya Israel ingekuwaje.

Maana NATO, EU na mataifa yote ya magharibi wanatoa msaada wa silaha, kiuchumi na kidiplomasia kwa Ukraine lakini bado Urusi anasonga mbele kuteka maeneo, Leo hii Ukraine haiwezi anzisha counter offensive maana haina tena askari wabaotosha, waliopo ni kupunguza kasi ya Urusi kwa kuzuia mashambulizi (ambao pia hawatoshi), Kazi yao nyingine ni kufanya ugaidi ndani ya ardhi ya Urusi.
 
So far Ukraine imepewa msaada wa silaha wenye thamani ya USD billions ngapi kutoka nchi wanachama wa NATO plus mercenaries na mafunzo?​


Russia , zaidi ya makombora yake ya nuclear, hana chochote cha pekee. Ndiyo maana wataalam wa masuala ya vita, wanasema uwezo wa kijeshi wa Russia ulikuwa exagerated.

Ukraine iliweza kuizuia Russia kuitwaa Kiev bila ya msaada wowote kutoka mataifa ya Ulaya. Misaada ya fedha na silaha imekuja baadaye wakati tayari wanajeshi wa Urusi wakiwa wamefurushwa toka Kiev na kwenda upande wa Mashariki.

Russia imetepeta mpaka kuomba kusaidiwa na North Korea, na wapiganaji binafsi toka India na nchi nyingi za kiarabu.

Urusi katika uwanja wa vita, ni ya kawaida tu.

Military and war experts agree that perceptions of Russia's war capabilities have been exaggerated, particularly concerning its ability to win the war in Ukraine, which has revealed significant weaknesses in its military-industrial base, command structure, and professional units. Key indicators include reliance on Soviet-era equipment, failure to modernize, high casualties, slow territorial gains relative to losses, and a struggle to replace components or build new technologies. These realities contrast with historical Russian military defeats and underscore the impact of sanctions and Ukraine's resolve, challenging the notion of Russia's inevitable victory, according to the Atlantic Counci.
The Russian military has suffered significant losses in personnel and equipment. Its performance has been hindered by a rigid command and control structure, a weakened corps of trained and professional units, and a reliance on tactics that have contributed to high casualty rates.

Russia's invasion of Ukraine had produced β€œmore harm than benefit,” and cited human suffering and the loss of life.


Urusi ni dhaifu sana kwenye uwanja wa vita. Urusi imewahi kutandikwa na Japan, imewahi kutandikwa na Finland, ikasalimu amri.

Russia also suffered defeats, such as during the Russo-Japanese War and the Winter War against Finland.
 
Mkuu unavyosema Urusi ni dhaifu mbona USA, NATO naye na vibaraka wake wa Magharibi mbona hawaiachi Ukraine ipambane yenywe bila kutoa msaada wa zana za kijeshi, intelijensia, kidplomasia?

Na kama kweli Urusi ni dhaifu kwa nini Ukraine hasiongi mbele kukomboa ardhi yake na kuimaliza Urusi?


USA, EU na NATO wote sasa wanaitaka Urusi ikubali mazungumzo, Zelensky aliyedai kuikomboa Ukraine yote kwa nguvu za kijeshi leo hii haamini kuwa hawezi fanya counter offensive tena.

Yani adui dhaifu amevuka mpaka anaikalia ardhi ya Ukraine, pamoja na udhafu wote huo, Ukraine imara yenye silaha bora za USA, UK, Ujerumani, Ufaransa nk... lakini bado haiwezi kumfurusha Urusi iliyo dhaifu?
 
😁😁😁😁
 
Kutoiadhibu vipi wakati wamezidungua? Ndo adhabu ipo hapo. Imenishangaza hadi Poland ana mdindia Mrussi? Mrusi anaanza ku fail sana.
So ulitaka waziache zipite katika anga lao , kama kweli Poland wame vurugwa na wao watume drone zao zipite ktk anga la Russia
 
Kawaida tu hiyo. Mbona hata sisi Tanzania tulimvimbia marekani. Ni kutafuta kiki tu ili nchi nayo ikumbukwe. Kuna nchi unaweza kuzisahau kama zipo endapo kusipokuwa na sababu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…