Pole dada yangu Damie kwa kufiwa na baba yako mzazi

Pole dada yangu Damie kwa kufiwa na baba yako mzazi

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
8,169
Reaction score
3,351
Kwa masikitiko makubwa sana napenda kumpa pole mwanaJF mwenzetu Damie kwa kufiwa na baba yake mzazi. Najua upo katika wakati mgumu lakini Mungu akupe ujasiri katika kipindi hiki kigumu.

Najua utakuwa upo katika harakati za kujiandaa kwenda nyumbani kwa ajili ya mazishi, Mungu akutangulie ufike salama.

Pole sana Damie.

Inallilaah wainarajiun,

Bwana ametoa na Bwana Ametwaa, jina lake libarikiwe.
 
Aisee! Dah!

Pole sana Damie. Mungu akupe moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu sana kwako.

RIP mzee wetu.
 
Pole Damie....Mungu akupe wewe na jamaa wote FARAJA kuu.
 
Poleni sana kwa msiba, Mwenyezi Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe, Mzee wetu alale pema peponi -Amen
 
Poleni sana wafiwa lakini kumbukeni tu kuwa KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA!!! BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
 
Asanteni nawashukuru. Kazi ya mungu haina makosa. Baba ananiumiza sana mwenzenu.
 
Inna lilahi wa Inna Illahi rajjunn. Pole sana ndugu Damie na familia yako kwa msiba huu. Be strong and find your recomfort in the idea that we will meet again. My deepest sympathy...
 
Roho ya marehemu ipate rehema kwa Mungu, apumzike kwa aman, Amen! Pole sana mpendwa!
 
Kwa masikitiko makubwa sana napenda kumpa pole mwanaJF mwenzetu Damie kwa kufiwa na baba yake mzazi. Najua upo katika wakati mgumu lakini Mungu akupe ujasiri katika kipindi hiki kigumu.

Najua utakuwa upo katika harakati za kujiandaa kwenda nyumbani kwa ajili ya mazishi, Mungu akutangulie ufike salama.

Pole sana Damie.

Inallilaah wainarajiun,

Bwana ametoa na Bwana Ametwaa, jina lake libarikiwe.

Asante nashukuru nk safarini kuelekea kwa mazishi.
 
Pole sana Damie,
Ila Mzee wa Rula amekuruhusu kutaja identity ya Mzee wake, maana tayari umeshamu expose mwenzio.
 
Pole sana Damie mungu azidi kukutia nguvu. Na ulinzi mwema katika safari.
 
Siku nyingi sijamuona jamvini. . .
Pole mwaya!!!
 
Back
Top Bottom