Pole kwa kufunga

Pole kwa kufunga

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
POLE KWA SWAUMU.


1)Japokuwa nalegea,ila katu sitochoka

Siku nazo zakimbia,taratibu zaondoka

Hazito tusubiria,kwa kasi zitaondoka

Ndugu msinipe pole,sijachoshwa na swaumu



2)Pole zenu nachukia,mwenzenu ninakereka

Mi tiba najipatia,afiya kutengezeka

Sa pole mwaniambia,sitaki kuwaitika

Ndugu msinipe pole,sijachoshwa na swaumu.


3)Imani natafutia,sitaki kutetereka

Hasira yanipandia,kwa ndàni natetemeka

Nyinyi kutwa mwajilia,mi nataka neemeka

Ndugu msinipe pole,sijachoshwa na swaumu.



4)Kidogo kijikondea,afiya kuimarika

Siyo kujinenepea,mwili kupata gharika

Nishindwe hata tembea,naona mmechezika

Ndugu msinipe pole,sijachoshwa na swaumu.


5)Sipendi kuisikia,pole mkiitamka

Msidhani natulia,bado nimechangamka

Kwa Rabi ninatubia,imani sije anguka

Ndugu msinipe pole,sijachoshwa na swaumu.


6)Thawabu najisakia,toka kwa mumba Rabuka

Funga ninajifungia,siyo nimekurupuka

Vitabu vinatwambia,siyo jambo la kuzuka

Ndugu msinipe pole,sijachoshwa na swaumu.


7)Funga nimekusudia,imani kusafishika

Maaswi naogopea,sitaki kushawishika

Njaa nikajishindia,hasara ikanifika

Ndugu msinipe pole,sijachoshwa na swaumu.

SHAIRI- Pole kwa Swaumu.

MTUNZI-Idd Ninga,Arusha

iddyallyninga@gmail.com

+255624010160
 
Kufunga swaumu raha sana Mungu atujaalie ktk mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Ramadhani kareem.
 
Back
Top Bottom