Pole mvulana

Pole mvulana

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
27,970
Reaction score
35,168
Hii nime copy na kupaste:

Mvulana mwanafunzi alimwambia baba yake kuwa siku hiyo alikuwa anajisikia kuumwa hivyo hawezi kwenda shule. Baba akamwambia poa apumzike.

Baba kazi yake ni Bodaboda.

Muda wa mchana baba akapata abiria binti mrembo, akamwambia ampeleke guest house X. Akamwambia yule bodaboda kuwa wakifika mwisho wa safari, mwenyeji wake atamlipa hela ya usafiri hivyo asiwe na shaka.

Walienda hadi kwenye ile guest house, bi dada akampigia simu mwenyeji wake aje alipe hela ya usafiri.

Mwenyeji wake alikuwa ni yule mvulana ambaye alisema haendi shuleni kwa kuwa anajisikia kuumwa.

Mvulana akatoka ndani kwenda kumlipa bodaboda, Lahaula akakutana uso kwa uso na baba yake mzazi.

Kilichotokea baada ya hapo, nitaendelea baadae...
Castr masara njooni huku muone mambo ya wavulana
 
Umenikumbusha #MarkAngelComedy kama ilivyo.. Sema mshua alimleta demu wa mwanae mpaka nyumbani kwake (baba)...
 
Back
Top Bottom