Pole siwezi toa, bila masahibu kujua
Mengine tumezoea, uchao yatokea
Tafadhari elezea, lipi limemfikia
Bado Pole yangu naihifadhi, mpaka nijue yaliyomsibu
Mengine si janga, bali kuanua tanga
Labda la upanga, hapo Mola hajapanga
Moyoni sina gamba, na wala si tenga
Bado Pole yangu naihifadhi, mpaka nijue yaliyomsibu
Kuna ya kuugua, na ya kuuguza
Uzito hupungua, kulingana na bughudha
Iweje pole sawia, kwa yasiyo bebana
Bado Pole yangu naihifadhi, mpaka nijue yaliyomsibu
Chonde nieleze, nisiendelee hifadhi
Nalijua zeze, yatapona hata maradhi
Hizi si kelele, bali nataka ukweli
Bado Pole yangu naihifadhi, mpaka nijue yaliyomsibu
Nitarudi tena, utu kutekeleza
Naijua milima, katu si kama nabeza
Sharti sema, kipi kimetokea
Bado Pole yangu naihifadhi, mpaka nijue yaliyomsibu