Pole sana Freeman Mbowe, hongera kwa kuwa huru na Asante!

Pole sana Freeman Mbowe, hongera kwa kuwa huru na Asante!

SUTAGI-

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2018
Posts
278
Reaction score
515
1. Pole sana Mheshimiwa Mbowe kwa kukaa rumande kwa kipindi hicho chote. mambo mengi ya kifamilia, kiuchumi, kijamii na kisiasa yalikwama kwa sababu haukuwepo mtaani.

Sisi wafuasi na wapenda haki tuliumizwa sana kwa kuwa ilikuwa ni unyanyasaji wa wazi wa dola dhidi yako na wenzako bila hata chembe ya aibu.

Mungu atawalipa ktk hayo mliyopitia.

2. Hongera sana kwako na wenzako kwa kuwa mmeachiwa bila masharti na upande wenye dola umedhihirisha kuwa kesi yenu haikuwa na mashiko. Kwa maana nyingine wale wote waliojigamba na kukuchafua kabla hata ya kufika mahakamani wana deni kubwa la kulipa.

Kwa nchi zilizoendelea ktk mawanda ya demokrasia na uwajibikaji, leo hi viongozi kadhaa wangeachia nafasi zao.

3. Asante Mbowe na wenzako kwa kuwa kesi yenu imewafungua Watanzania wengi. Binafsi kila kesi iliposomwa nilikuwa nafuatilia kujua yaliyojiri.

Asanteni Mawakili Wasomi kwa kusimama kidete na kusimamia haki hata pale mlipooneshwa upendeleo wa waziwazi.

Zaidi ya yote Asante mhabaroshaji wetu uliyeweza kuandika neno baada ya neno kutoka mahakamani ukaweza kutuhabarisha sisi wananchi tuliotapakaa kila kona ya Dunia. Mungu atakulipa

Mwisho: Tuendelee kuchangia Chama kupitia ajenda ya Join the Chain, One Million Challange
 
Inspekta swila

Luteni denis urio

Acp kingai

Inspector ndowo

Inspector mahita

Wazee wa ku connect dot waliudanganya umma kwamba MBOWE ni gaidi wawajibishwe kwa maslahi mapana ya jeshi la polisi na umma wa watanzania
 
Ila watu Wana maana hasa Hawa wachonga mchongo
 
Back
Top Bottom