OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Twende kwenye hoja moja kwa moja.
Chadema iliwapa fursa wanawake takribani 60 kugombea kwenye majimbo mbalimbali. Miongoni mwao walikatwa kikatili na bila sababu na tume ya Taifa na kunyimwa fursa ya kugombea. Miongoni mwao ni waliokuwa wabunge Suzan Kiwanga na Lucy Owenya. Tena basi kabla ya hapo kuna kundi kubwa la wanawake waliondolea kugombea baadaye wakapambana wakarudi.
Katika muktadha wa kuheshimu nafasi wanazopewa wanawake,Humprey Polepole alikuwa wapi kukemea ukatili huu dhidi ya wanawake? Wako wanawake waliodhalilishwa sana wakati wa uchaguzi kwa kupigwa na kutukanwa na wagombea wa chama chake. Humprey alikuwa wapi kukemea uzandiki huu ndani ya chama chake.
Tunajua hili mna maslahi nalo,lakini ushauri wa bure basi jitahidini kutumia vizuri busara na akili. Mnaidhalilisha sana nchi na kutufanya wote tuliomo tuonekane maboya,kumbe ni kikundi kidogo tu cha watu.