Polepole: Magereza ni wazalishaji na tuliwaunga mkono ili wapandishe bendera za CCM mitaani na risiti ya malipo tunayo

Nilitegemea hili jibu.
Hata kwenye comment yangu nilisema hivyo hivyo.
Sasa tusubiri na jibu la polisi kufanya kazi za tume..
 
Jifunze kwanza kuelewa ndipo uje hapa

Kama unashindwa kuelewa kuwa magereza wanafanya uzalishaji sasa utaelewa mambo makubwa?
Ndo maana nokakuambia wadanganye wajinga wenzio ccm..ni wajinga tu ndo watakuelewa
 
Na polisi kushusha bendera za upinzani mnawaunga mkono ktk uzalishaji?
 
Chama kinachopendwa hakiwezi kutumia pesa kupandisha bendera.. wanachama hujitolea wenyewe bila malipo yoyote! Hii inaendelea kudhirihisha kuwa ccm haipendwi! #Ukitoa risiti ya kupandisha utoe na ile ya polisi walivyokuwa wanashusha bendera za chadema kule same!#
 
Wangekuwa wanapandisha bendera za Chadema au ACT RPO angebaki na hiyo nafasi? shame on him
 
Wamebaki kutumia dola pekee
 
Sinto acha kumshukuru Mw.Nyerere kwa kunisomesha BURE KABISA mpaka namaliza chuo.
 
Kwa hiyo ukipandisha bendera hapo unakuwa umezalisha kitu gani hasa....
 

Wamenunua watu na hasa wapinzani, sasa wamefikia kuwanunua watu walio chini ya taasisi/idara zilizo chini ya serikali, wakijua kuwa hao viongozi wa hizi taasisi/idara hawawezi kupinga.

Hiyo ndiyo ccm msiyoijua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…