Polepole uliahidi kufichua yanayoendelea kwenye usafiri wa mwendokasi, huu ndio muda mwafaka

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, aliwahi kusema kupitia njia ya mtandao kwamba atafichua uozo uliopo ndani ya mradi wa mwendokasi. Kauli hiyo bado inabaki vichwani mwa watanzania wengi, hasa wakati huu ambapo huduma za mwendokasi zimekuwa zikilalamikiwa kwa changamoto mbalimbali.

Wananchi wamekuwa wakilalamika kuhusu msongamano mkubwa wa abiria, uchelewaji wa mabasi, pamoja na hali mbovu ya usimamizi wa huduma hiyo muhimu ya usafiri jijini Dar es Salaam. Katika mazingira haya, wengi wanaona sasa ni muda muafaka kwa Polepole kutimiza ahadi yake ya kueleza kwa undani kile kinachoendelea, ili umma upate kujua ukweli na kuchukua hatua stahiki.
Your browser is not able to display this video.
 
Hata asemeje hakuna wa kuwajibika iwe viongozi au wananchi
 
Reactions: Lax
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…