Polepole usimlazimishe Rais kuleta Katiba mpya

Mhhh!!!!@lizaboni mpe kadi mpya huyu
 
Wengi wetu humu tumezaliwa kuanzia miaka ya 80_2000 katiba ya 77 tumeikuta rasimu ya kwanza ya katiba mpya tumepoteza zaid ya billion 27 badala ya kuiendeleza tunataka fedha zile zipptre bure.ccm acheni kuogopa nchi ni ya watanzania wote na wote tunataka katiba mpya kama nchi haina fedha watanzania tuchangishwe tutazitoa
 

Polepole halazimishi chochote. Sidhani kama ushiriki wa Mzee Warioba kwenye kampeni za uchaguzi wa 2015 baada ya kutukanwa sana na kudhalilishwa na makada wa ccm ulikuja hivi hivi tu. Bila shaka kulikuwa na ahadi nzito. Kitendo cha kuwavuta karibu baadhi ya wajumbe wa Tume ya Katiba mpya nacho siyo cha hivi hivi tu. Jambo moja lipo wazi pia kuwa Rais wetu hana lugha ya kidiplomasia. Hata hii ya kunyoosha nchi siyo lugha nzuri. Ndiyo maana mara kwa mara wasaidizi wake hujitokeza kufafanua matamshi yake muhimu ili watu wapate ujumbe ambao wanaamini ndio uliokusudiwa.
 
Hivi Polepole ana umri gani? huwa nashindwa kumkadilia hata rika lake maana yupo kama popo tu mzee si mzee kijana si kijana basi ni shiiida tu.

Ni kijana lakini ana sura na akili ya kizamani.
 
Wewe ndo hujaelewa.
Atawaachia mchakato huo kipindi Chake cha mwisho cha utawala wake 2025 [emoji23]
 
Aliyeipindisha nchi ni nani? Yupo hai au alishakufa? Hatua gani kachukuliwa?

hahahaha aliyepindisha ni hao CCM. Sijui wanainyosha ili kuwa haijapogwa pasi na watangulizi wake.
 
Inaonyesha muda si punde Tanzania itakuwa imenyoka toka dar mpaka hororo dar mpaka tunduma ni rula kwa kwenda mbele kama sivyo basi tujue anayosha wapi na kivipi?

Kama anaubavu ajinyooshe Mwenyewe. Mwizi ni mwizi tu,haoni yale madeal yake ya Kivuko kibovu duh!Kweli uke usemi toa kwanza boriti ndipo uone Kibanzi kinafanya kazi Kweli Kweli.
 
Sione kosa la Polepole anapoongelea mambo yanayo husu Nchi na Chama chetu sivema kubeza kila maoni na kiongozi yeyote hasa wa Kitaifa hata kama umeona hujaguswa na alichoongea tusipende kujenga majibizano yasio weza kujenga wala kusaidia chochote kwa Taifa letu !Katiba ya Nchi haipaswi kuwa na utikadi fulani yeye ndie anajua kwanini aseme hili la Katiba naje Rais akikubali kuna wakukataa?Tutoe Nafasi kwa wahusika watajadriana wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…