polepole ni mwanaharakati aliyejaliwa uwezo wa kutoa hoja hadi ukawa convinced kabisa, hata kama hoja ni ya kupikwa. bahati mbaya sana sijajua kabila lake, lakini ni mwanadamu anayependa sana sifa na kuonekana mbele za watu, ni mtu ambaye anajua hakuna mwenye uwezo au akili zaidi yake na anapoongea huwa anajiona yeye kama ndio final reference hapa duniani. kiburi hiki ndio huwa kinanifanya nibadilishe stesheni ya tv akiwa anaongea, anakera sana sana kumsikiliza.
nakumbuka kuna mdahalo mmoja ulishawahi kufanyika nkruma udsm wakawa wamemsahau kuwa msemaji wa mwanzoni na mwezie yule wa zenji, walipompa mike mwishoni alitaka kugoma asiendelee akatoa malalamiko kuwa amesahauliwa manake amekuja kupewa mwishoni wakati ambao hataongea mda mrefu na watu wakamwona kwenye tv. kijamaa kinakera sana sana.