Polepole utakuwa umechanganyikiwa


laiti ungejua haya yote usingesema, any way kamnyonyeshe mtoto analia.
 
laiti ungejua haya yote usingesema, any way kamnyonyeshe mtoto analia.

Tuwe wapole jamani, hapa tunataka tuelimishane vizuuuri ili mwisho wa siku mtamanyali ukapata elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa. Hiyo ndiyo hasa msingi wenu wewe na UFO-ALLIEN. Ili mjadala wenu uwe mzuri punguza jazba mtafika pazuri. Nami nakuasa ndg yangu Tanzania wewe na mimi tunaijengea historia gani kupitia Katiba? Isome kwanza na jiandikishe muda ukiwadia kapige kura!
 
Katiba pendekezwa inawachapa wenyewe....wameondoa vipengele vya Warioba...sasa imemchapa WASSIRA kwa kufanywa komedy...kafunga tenge koti lake.

Ndugu kama we umesoma basi ishia hapohapo na mawazo yako mgando the beliave of all what has been written o said bila kuchanganya na zako wewe...inaelekea wewe ni google affected on ua studies....haiwezekani ukawa na vipengele vinavyogusa kila hali ya mzee leo uje uingize hadi hiyo vumbi la polepole lisilo na maana....nani kakwambia wazee wanahitaji hilo....mzee anahitaji huduma bora za matibabu..nenda kanda ya ziwa waulize wanamatatizo gani..hasa kweny mambo ya kishirikina....waulize wazee adha wanayopata hasa kwenye public transport....kaka nenda katika ibara ya 58 ya katiba inayopendekezwa kaisome halafu urudi hapa au uende kwa polepole akakwambie kingine ulete humu
 

Hute, nenda kanyonyeshe mwanao mchanga naona unawashwa na chuchu. Polepole siyo saizi yako.
 
Kwahiyo unataka iweje?


mbona rasmi ya wananchi imeeleza vyema vipi wananchi wangelipenda muungano wetu uwe.

warioba na tume yake walipewa kazi ya kukusanya maoni na walieleza iweje, au ww ndio hujaisoma?

kiufupi itambulike kua muungano wa nchi mbili zenye hadhi sawa.

mambo ya muungano ya punguwe na yawe na usimamizi wenye uwiano. hayo mapambio haki za wanawake, matumizi ya ardhi na mengineyo hayana maana yyte kwenye katiba ya muungano. maana zanzibar ina utaratibu wake wa kuyatungia sheria na kuyatekeleza kwa mujibu wa baraza la wakilishi na serikali ya mapinduzi
 

Ndugu mi nakushauri ukasome Katiba Inayopendekezwa vizuri kabisa katika Ibara ya Kwanza na ile ya Pili na vipengele vyake vyote utapata kuelewa jambo muhimu juu ya kitu unachokizungumzia hapo juu.
 
BONGO ndio nchi pekee wataalam wanabishiwa na wapiga porojo mitandaoni.

Dah kweli mkuu watu wenye uwezo mkubwa kiakili na kufikiri wanapigwa madongo eti kwasababu tu wanaenenda tofauti na itikadi ya watu fulani. Hakika watu hawa waliiridhia demokrasia pasi kuijua undani wake. Wanachotaka ni kuendelea kuamini mlengo wa "ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI". Hayo mambo yashapitwa na wakati kila mtu anaweza(anahaki) ya kuyapima mambo ya kitaifa kwa uwezo wake ilimradi tu asivunje katiba na sheria za nchi. Anyway leo kwa mara ya kwanza nabahatika kukutana na GREAT THINKER Humphrey Polepole kama kawaida katika ubora uleule ataendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wa Saut- mtwara kuhusiana na rasimu ya mwisho ya katiba inayopendekezwa. Muda nia kuanzia saa 3:00 asubuhi. Mungu ambariki sana huyu kijana.
 
Ndugu mi nakushauri ukasome Katiba Inayopendekezwa vizuri kabisa katika Ibara ya Kwanza na ile ya Pili na vipengele vyake vyote utapata kuelewa jambo muhimu juu ya kitu unachokizungumzia hapo juu.


sijui niisome mara ngapi, hata uniamini, kwanza sikubaliani na ibara ya 2 -2 rais wa tanzania asiwe na mamlaka kabisa ya kuigawa zanzibar kwenye mikoa. mambo ya kuweza kukasimu iondoke na mamlaka ya kuigawa yabaki kwa rais wa zanzibar ikiwa vile inabakia lile tulilolikataa kua Tanganyika wanatukoloni.

mm pia sikubaliani na ibara ya 9. hii ni ile ile kuliweka chini baraza la wakilishi na serikali yake na kuipaisha ya muungano. nnasisitiza muungano lazima uwe wa usawa na kuheshimiana na sio mmoja kujipa ukuu na mwengine kua mdogo big hapana

kwa hio hadi hapo panatosha kukupa picha ni kipi hasa tunachosimamia
 

Sasa Sheikh weye watoka Pemba au Kiembesamaki? hilo suala uloliweka mahala hapa ni lako we binafsii, sio kila kitu kwenye Katiba kitaandikwa vinginevyo kila mtu angependa iandikwe kwa mtindo anaoupenda yeye jambo ambalo haliwezekani, tukubaliane na haya sheikh!!
 

mm ni mzanzibari wapi natoka si muhimu

tuliungana tukiamini ni nchi mbili huru. katiba inaonyesha kuna Tanzania ambayo kwa udhati ni tanganyika na zanzibar ambayo inaonekana kama ni subdivision ya tanganyika hilo big nooo

sisi tulitaka muungano wa serikali tatu ili kila upande uwe huru kufanya yake na kubakiza yale machache tuyafanye kwa pamoja na kwa muundo wenye uwiano sawa.

michezo si muungano katiba haijajibu suali kwa nn TFF wawe na mandate ya kuwakilisha zanzibar kwa mwamvuli wa muungano ? vp ZFA

kilimo si muungano iweje FAO wende bara na wawe wanachama zanzibar isujudu kuomba kupitia bara ? hili katiba hawajalijibu

afya si muungano kwa nn Tanganyika wavae koti wajiwakilishe na zanzibar ihemee kwa kuomba huruma ya tanganyika?

mambo ya biashara na sera za biashara kwa nn ziamuliwe na Tanganyika kwa mwemvuli wa muungano ?

siipigii na sishawishiki kamwe kuuza thamani ya mapinduzi ya 64 waliopigania wazee wangu. muungano huu sio na katiba hio sio tunayoitaka haileti hadhi ya zanzibar na inaikweza zaidi Tanganyika big noo
 
Ndugu mnaochangia kwenye JF kuweni wastaarabu. Natumaini kuwa hili jukwaa la watu wenye level fulani ya kuheshimika katika jamii. Sasa unavyoanza kuporomosha matusi unanikumbusha hadithi ya makuli na pengine baadhi ya wabeba zege. Hao kuachia matusi wanaona ni kawaida. Muda wa kuandika matusi utumie kusoma na kuelimisha wenzio kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Ukitukana unajishushia hadhi. Halafu unadhani kwa kutumia kijina chako hicho kwamba ndo umejificha no tunakufahamu. Ili uendelee kuheshimiwa katika jamii acha tabia hiyo, badilika na jenga hoja. Nimekuwa nikikwambia kama huwezi kujenga hoja njoo nikufundishe bure. Umesikia wewe unayeongea matusi!!!
 

Sheikh sheikh punguza nchechetoooo!! wala hutakiwi kupanick, kumbuka kuwa kura ni siri yako, hapa si mahala pakuja kutambishana kuwa wewe utapiga kura ya aina fulani, nasisitiza kuwa kura ni siri yako wewe mwenyewe, kitu kingine tayari nimekwambia si kila jambo lazima liwepo kadri mtu atakavyo, tukifanya hivyo basi Katiba hii ingelikuwa ni zaidi ya magunia na magunia ya kurasa zenye kuwekwa kila jambo atakalo na alipendalo mtu. Kuwa muungwana ndo imeshatokea hivyo, lakini mambo mengine uloyaweka hapo juu hayana ukweli wowote labda uweke ushahidi watu tukuelewe ingawa naamini hauna huo ushahidi. Ni hayo tu Sheikh
 


nazani mwenye kupaswa kuweka ushahidi ni wewe unaesema mengine hayana ukweli.

ama kura ni siri lkn nnaweka sawa ile kauli tulioanzia mjadala kua hii katiba ni nzuri hii katiba kamwe si nzuri na hatuwezi kusema ishatokea tuikatae tuifumue tuje na katiba itayoleta maslahi kwa wananchi wote wa pande mbili za muungano.

mm sijapanick kabisa, ulinitaka nisome sura ya kwanza na ya pili nimesoma na kukueleza. sasa ww nenda kasome sura ya nane nioneshe mamlaka ya rais wa zanzibar kwenye muungano ?

yy kama garasa tu hazidishi wala hatoi, hilo big noo. tunahitaji kuona nchi hizi mbili zinajisikia fahari juu ya muungano huu. tuache hili la kudogoshana na kukandamizana.

muungano twautaka hela usitudonyowe
 

Sheikh hilo suala lako la kutaka ifumuliwe naomba ulisahau na hii katiba ndo yenyewe, kama hupend basi tafuta uraia nchi jirani naona Tanzania umeichoka.
 

Kuhusu hoja yako uliyoitoa ya "sasa ww nenda kasome sura ya nane nioneshe mamlaka ya rais wa zanzibar kwenye muungano ?"


Rais wa Zanzibar kwenye Katiba Inayopendekezwa nafasi yake ameainishwa kama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Ibara ya 99. (b) Inayoainisha kwamba Rais wa Zanzibar atakuwa Makamu wa Pili wa Rais kati ya Makamu wa Rais watatu.


Nimependa namna yaako ya ushiriki katika kuelimishana kuhusu jukumu la kuijua Katiba Inayopendeklezwa kama raia wanaoipenda nchi yao. Ni muhimu kujua mambo mengi badala ya kudanganywa na wtu wachache wenye nia mbaya na nchi yetu.
 
Tatizo la wana jf ni moja mnakomaa kusoma katiba inayopendekezwa peke yake wakati mna nondo tatu za kusoma labda niwasaidie...someni katiba ya 77 theni someni mapendekezo ya warioba halafu someni katiba inayopendekezwa hapo ndipo mtaona utamu wa katiba inayopendekezwa....waulizeni watu wenye ulemavu....wasananii...wakulima jinsi walibyominywa kwenye Rasimu ya mzee warioba ila kutokana na bunge maalum la katiba....waliweza kuongeza vifungu ambavyo kwenye katiba inayopendekezwa vimeingizwa..

N:B
Sitaki matusi if u hav concern toa hoja uelimishwe....vijana tusipotoshwe na tusiwe wavivu kusoma....
 
Hute, nenda kanyonyeshe mwanao mchanga naona unawashwa na chuchu. Polepole siyo saizi yako.

Mkuu naamini katika maneno yako. Polepole si size ya mtoa mada, leo katushushia nondo mpaka mtu unatamani kuwa yeye. Mungu ambariki sana Humphrey Polepole.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…