Polepole utakuwa umechanganyikiwa


ukiacha kutajwa tu kuwa atajulikana kama ni makamo wa pili wa rais, yepi mamlaka yake kama mshirika wa muungano?

nimesoma sikuona, hana nafasi yeyote ya uteuzi watendaji wa muungano, hana hata nafasi ya kushauriana na rais wa jamhuri katika kuteua yeyote au kumfuta kazi yeyote. hana mamlaka hata ya kuongoza vikao ikiwa rais au hata makamo wa tatu hayupo.

haya ndio tunayoyasema zanzibar katiba hii hatuhiitaji ina mapungufu mengi.

kuna mmoja yeye anasema kua nafasi ya kuirekebisha hamna ila kuikubali tu , kama ni hivyo basi hii kurea haina maana yeyote ile. lakini mimi siamini hivyo inahitajika wananchi tukae kuichambua na kuyaona mapungufu haya na mengine kisha tupige kura ya hapana ili tupate mda wa kuja na katiba bora itayoondosha malalamiko ya pande mbili za muungano

katiba bora isio na malalamiko na itayokidhi shauku kuu za wananchi ndio itakayoleta maendeleo ya haraka kuliko hii ya bora liende. katiba inayotukuza utawala na ukoloni wa upande mmoja

mm kura yangu ni hapana. na kama mzanzibari nnasema "sio moja sio mbili bali mamlaka kamili"
 
Ndugu yangu Mtu waPwani hongera sana kwa kutaka kujua mambo ya Katiba Inayopendekezwa. Unaulizia mamlaka ya Makamo wa Pili wa Rais kuwa ni yepi. Ukisoma Katiba ya Zanzibar utakuta majukumu mengi ya Makamo wa Pili wa Rais ambaye ndiye Rais wa Zanzibar. Hivyo isingekuwa busara mtu yule yule kurundikiwa majukumu mengine upande wa Muungano. Ndo maana haya majukumu Katiba imewaachia wasaidizi wengine wa Rais. Kwa elimu hii ninayokupatia endapo utakuwa ni mwenye kutaka kuelewa na kubadilika, basi jiandae kuongea Kuwa Yako ya Ndiyo kwa Katiba Inayopendekezwa. Ukiwa na swali jingine karibu sana utaelimishwa tena buree. Wabillah Tawfiq.
 
Umeelewa somo Mtu wa Pwani! Ukimya huu unaonyesha kuwa umeelewa.
 
Umeelewa somo Mtu wa Pwani! Ukimya huu unaonyesha kuwa umeelewa.


ningependa uniorodheshee vifungu vinavyoonyesha kazi na majukumu ya rais wa zanzibar kwenye muungano ukiacha kuhudhuria baraza la mawaziri?

sisi tunaona mtu ambae anapaswa kumshauri na kushauriana kwenye mambo ya muungano ni rais wa zanzibar mamlaka hayo hana. pia hakupewa hata sauti ya kua na kura ya turufu alau kwa yale ambayo atayaona kua hayana maslahi kwa zanzibar

bado katiba haijaitendea haki nafasi ya rais wa zanzibar kwenye muungano na kwa hio nnasisitiza kura ya hapana ndio suluhisho
 


Kura ya turufu?
 

Kaka uspende kukurupuka na kudai hiyo kura yako ya hapana ama kuhamasisha watu kupiga hiyo kura, Katiba Inayopendekezwa imeainisha mambo kuhusu Rais wa Zanzibar ukiacha hilo ulilolisema hasa katika ile SURA YA 11 IBARA YA 164.
 

HAO TAYARI WAMESHAPEWA LAWAMA NA NADHANI MESSAGE ZIMEWAFIKIA KUWA WAO HAWAPASWI KUINGILIA MAMBO YA SIASA, WAENDELEE NA MAMBO YA DINI. Khaaaa!!
Kama hawa takiwi kuingilia mambo ya siasa mbona wame pewa nakala za katiba pendekezwa na Nina kuhakikishia kuwa kama viongozi hawa wa dini wange waambia waumni waipigie kura ya ndiyo wagepongezwa na serkali mpaka wange andaliwa hafla ya kuwa pongeza AKILI MUKICHWA
 

bahatikisiya, wananchi wote wanapaswa kupewa na kuisoma Katiba Inayopendekezwa bila kujali dini, kabia na matabaka mengine maana hayo siyo hata msingi wa katiba hiyo. Kwa kuw wao pia ni Watanzania ni haki yao kupata nakala ya Katiba Inayopendekezwa kulingana na utaratibu ulivyopangwa kwnye maeneo yao. Nawe tumia fursa hiyo ambayo ninatamani kila mtu apate nafasi ya kuisoma katiba inayopendekezwa ili aweze kufanya maamuzi sahihi.
 
Wamepewa ili wajue kuwa hata haki zao zimo kama taasisi za kidini, wewe ndo umekosa akili hapo unadhani wamepewa mapambo yale? Khaaaaaa aibu hiyo yani we unawaambia wenzio eti akili mukichwa wakati wewe ndo umechemka hapo.
 
Kaka uspende kukurupuka na kudai hiyo kura yako ya hapana ama kuhamasisha watu kupiga hiyo kura, Katiba Inayopendekezwa imeainisha mambo kuhusu Rais wa Zanzibar ukiacha hilo ulilolisema hasa katika ile SURA YA 11 IBARA YA 164.


kaka tujadiliane kwa heshima na adabu ili tufaidike, sizani kama sawa kutumia lugha ya dharau na kejeli. mm nnasema kura ya hapana na nnajadili na kushawishi na wewe una haki ya kusema ndio na kushawishi ili tuone kweli kuna haja hio kwa heshima na utu.

turudi kwenye mjadala sura ya kumi na moja kwa ujumla wake inazungumzia serikali ya mapinduzi, baraza la mapinduzi la zanzibar na baraza la wakilishi la zanzibar. hapo unaona kua sura nzima haizungumzii mambo ya muungano, hayo ni mambo ambayo yanasimamiwa na zanzibar na tayari yeshaainishwa vyema kwenye katiba ya zanzibar kuyarejea hapa just ni kuongeza karatasi tu za katiba.

tuje kwenye ibara ya 164 ipo kwenye sura ya kumi na mbili na sio ya kumi na moja, lkn pia inazungumzia mahakama na uhuru wake, nimesoma kujiridhisha sijaona mamlaka ya rais wa zanzibar kwenye ibara hii.

nnachozungumzia mm muungano huu ni washirika wawili zanzibar na tanganyika zilizokua zenye mamlaka kamili ambao kwa hiari yao bila kushurutishwa wala kutenzwa nguvu wameamua kukubaliana sehemu ya mamlaka yao kuyasarender kwenye muungano. sasa iweje leo rais wa upande mmoja asiwe na sauti kwenye muungano huo?

suali langu bado nnataka kujua ni zipi kazi za rais wa zanzibar kwenye muungano ? kama zipo nnaomba mnionyeshe ukiacha kuapa na kuhudhuria baraza la mawaziri ?
 
ndugu yangu makubaliano ya muungano yaliosainiwa kati ya Marehemu JK Nyerere na Hayati Karume ni kua kuna mambo ya muungano na yasio ya muungano.

makubaliano mambo yasio ya muungano yote yatashuhulikiwa na nchi wenyewe na ya muungano yatashulikiwa na serikali ya muungano

sasa zanzibar wao wanaserikali yao na wanasimamia mambo ambayo si ya muungano, Tanganyika wao wakaamua mambo yao yasio ya muungano na ya muungano yasimamiwe na serikali ya muungano

sasa rais wa Muungano anasimamia ya muungano na ya tanganyika, hilo sisi hatuna la kusema maana watanganyika wameamua wenyewe kuyapeleka mambo yao yasimamiwe na chomobo hicho, lkn cha msingi mambo ya muungano tuyasimamie pamoja na ndio maana kwa wakati wao hakuna litalofanyika la muungano bila kusahuriana kwanza na rais wa zanzibar kisha ndio liamuliwe, role ya rais wa zanzibar ilikua wazi kua ndie mshauri mkuu wa rais wa muungano.

sasa katiba hii just imemuweka kuua soo tu, lkn hamna lolote la msingi analosimamia, rais anaweza kuchagua mawaziri, mabalozi, majaji na mengine bila hata kumshauri wala alau kumtaarifu rais wa zanzibar.

na kwa ilivyo sitashangaa rais wa zanzibar kusoma baadhi ya teuzi magazetini kama mm tu, jee huu ndio muungano ulio na usawa ?

MM KURA YANGU NI YA HAPANA
 
Mkuu naamini katika maneno yako. Polepole si size ya mtoa mada, leo katushushia nondo mpaka mtu unatamani kuwa yeye. Mungu ambariki sana Humphrey Polepole.

Ts all of ua thin thinking capacity....vijana kama husomi alwayz utaburuzwa na ndicho kinawakuta wandugu.....
 
Punguza jazba, eleza jambo lieleweke upate kujibiwa, usitukane, busara ni muhimu zaidi badala ya mihemko ya chuki, unataka kuniambia watanzania wote wanaelewa? twende tartiibu.
 

Bila shaka wewe sio mzanzibar...hivyo hujui hitaji lao lilikuwa ni lipi....waelimishaji huyu msinishane nae coz hata anachoongea hakijui....aanze kuchukua mapendekezo ya warioba na katiba inayopendekezwa asome ndo arudi hapa blah lah zosizo na maana hatutaki...unapoteza muda kuongea rubbish
 
Chuki tu hizo, tumia ndimu kama umechefukwa, Polepole ni kichwa ubadilishe chaneli au uache, mbona huku hujabadilisha mtandao? Kalia hiyo
 
Ts all of ua thin thinking capacity....vijana kama husomi alwayz utaburuzwa na ndicho kinawakuta wandugu.....

How about you too? Hapo wewe unaona umetumia usomi wako woooote kujenga hiyo criticism? Kama ndivyo, ngoja ustarabu wangu unifanye nisitumie weakness yako kupata dhambi nakaa kimya.
 




Hivi wewe Mtu wa Pwani
una matatizo gani! Huyu ni rais wa Zanzibar majukumu yake hayawezi kuonyeshwa katika Katiba inayopendekezwa. Majukumu yake yamo kwenye Katiba ya Zanzibar. Hicho unachokiona kwenye Katiba Inayopendekezwa

ndicho kinachomfaa. Mbona huongelei ya wale makamo wengine. Lete hoja nyingine hii kwako imeshagonga ukuta wa Zege.
 
Ukiona mtu anamjadili mtu hasa kwa chuki ujue unamkubali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…