Police Forensic art of facial reconstruction: FBI GENIUS wakiokota Fuvu (Mabaki) la marehemu wanaweza kulitumia katika kutengeneza taswira yake halisi

Police Forensic art of facial reconstruction: FBI GENIUS wakiokota Fuvu (Mabaki) la marehemu wanaweza kulitumia katika kutengeneza taswira yake halisi

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
POLICE VISUAL INFORMATION SPECIALISTS & FORENSIC ART OF FACIAL RECONSTRUCTION: FBI GENIUS wakiokota Fuvu (Mabaki) la marehemu wanaweza kulitumia katika kutengeneza taswira yake halisi.

images (1).jpg


Forensic Facial Reconstruction ( au Forensic Facial Approximation) ni njia inayotumika katika medani ya upelelezi wa Police pale ambapo uhalifu unahusisha mabaki ya mtu asiyetambulika. Hii facial reconstruction hufanywa na msanii/mtaalamu wa kuchora kama Masoud Kipanya (kwa kiingereza anaitwa Forensic Artist) ambaye amebobea haswa katika taaluma ya "facial anatomy".

Huyo mtaalam wa kuchora mara nyingi hufanya kazi kwa ukaribu sana na mtaalam wa mambo ya kale (Forensic Anthropologist) ili kuweza kutafsiri na kutambua sifa mbalimbali za skeleton au fuvu ambazo mwishoe zitasaidia kung'amua umri, jinsia pamoja na uzao wa marehemu.

Mtaalam huyo wa kuchora pia anao uwezo wa kutambua masuala mbalimbali kama vile umbo la sura ya marehemu (sura ya duara ama nyembamba), ushahidi wa majeraha kama vile jino au pua iliyovunjika kwa kipigo.

Utengenezaji wa taswira (Facial Reconstruction) huwapa wachunguzi na wanafamilia wanaohusika katika kesi za jinai zinazohusu mabaki ambayo hayajatambuliwa njia mbadala na ya kipekee wakati mbinu zingine zote za utambuzi zikiwa zimeshindikana.

Ukadiriaji wa taswira (Facial approximations) mara nyingi hutoa kichocheo ambacho hatimaye husababisha utambulisho mzuri wa mabaki kujulikana.

CASE STUDY ONE (1) MFANO WA TUKIO LA UHALIFU: Mauaji ya Mtanzania Mwivano Mwambashi Kupaza huko nchini Marekani.

Mama moja mzungu na watoto wake walienda kufanya picnic kando ya mto. Walikuta vipande vya maiti vimetupwa ndani ya mifuko ya takataka. Waliita polisi. Polisi walishangaa mambo waliokuta.

Maiti ilikuwa imechunwa ngozi, maiti imekatwa katwa viapnde kitaalamu hasa, lakini wali kuta kipande chenye nywele na kujua kuwa ni maiti ya mwanamke mwenye asili ya Afrika.

images (2).jpg


Polisi walichunguza database zao za watu ambao wamepotea. Hawakupata kitu waligonga ukuta. Waliomba msaada wa wataalam wa forensics kusudi wajue huyo mwanamke alikuaje.

Hata fuvu (skull) yake ilikuwa imebomolewa lakini waliweza kuijenga kwa kutumia kompyuta. Baada ya hapo walipeleka kwa mtaalamu wa kujenga uso (facial reconstruction) ndo ikapatikana hiyo picha ya hapo chini yenye taswira nne.

images (4).jpg


Polisi huko Wisconsin walisambaza hiyo picha sehemu nyingi na katika vyombo vya habari. Ndio mke wa Peter Kupaza na waTanzania wengine walipiga simu polisi na kusema kuwa hiyo picha inafanana na Mwivano Kupaza.

Pia mke wa Peter alimwambia kuwa huko Tanzania mume wake aliwahi kufanya kazi kama bucha na alimsimulia sana jinsi ya kuchinja mnyama na kumchuna ngozi. Hapo sasa Peter kawa suspect namba moja. Polisi waliwahoji sana waTanzania huko Wisconsin wakati huo.

Polisi walimfuata Peter nyumbani kwake. Kwanza Peter alidai hamjui Mwivano. Baadaye alisema kuwa alirudi Tanzania na jamaa anaitwa Shadrack lakini hajui jina lake la pili eti. Polisi wa Wisconsin walipiga simu Tanzania na kuambiwa kuwa Mwivano bado yuko Marekani.

Sasa ingawa Peter walimshuku walishindwa kumkamata kwa sababu walikuwa bado hawana uhakika kuwa hiyo maiti ni ya Mwivano. Wakati huo Peter alikuwa anafanya kazi kama 'Employment and job-training counselor for the Wisconsin Department of Labor and Human Relations'. Alivyondoka Tanzania alikuwa mwalimu.

Polisi walijua wasipokuwa wajanja kesi itaishia hewani. Walichukua mbwa wa kunusa nusa (sniffer dog) na aligundua damu chini ya mabao bafuni. Walifanya DNA Test na kugundua kuwa damu ni ya Mwivano. Lakini hiyo haikutosha kumkamata Peter. Kilichohakikisha kuwa maiti ni ya Mwivano ni kuwa Peter alimpeleka kliniki kutoa mimba! Hiyo mimba ilikuwa ni ya Peter.

Kumbe Peter alimgeuza ndugu yake mke mdogo. Mwivano alivyosign ile fomu ya kutoa mimba aliacha fingerprint. Ndo fingerprint hiyo waliomechisha na fingerprint kwenye maiti. Na mimi nasema roho ya kile kichanga kilichouliwa pale kliniki ndo kilimponza Peter Kupaza!

Peter alikamatwa na kesi ilipelekwa mahakamani. Huko mahakami Peter alidai kuwa Mwivano aliuliwa na mwanaume wa kizungu. Peter amefungwa maisha gerezani.

Lakini jamaa alivyo mshenzi alijaribu kukata rufaa. Lakini hataachiwa. Huyo Peter Kupaza ataoza gerezani.

NITAENDELEA NEXT TIME. NIPO SAFARINI NINAELEKEA IRINGA KUTATUA CHANGAMOTO ZANGU ZA KIKAZI.

OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Siasa?😳😳😳 How? Ben Saanane ni Binadamu anatafutwa sababu ni binadamu wewe unasema siasa?why? Uwe serious.jamaa kasema pasipo kuweka siasa.kasema atafutwe ben saa nane we unasema analeta siasa? Angesema atafutwe mwakipesile ungesema analeta ukabila? Angesema atafutwe abdallah ungesema analeta udini? Unataka aseme atafutwe nani? Mr Smith?

Mkuu, acha kuleta masuala ya kisiasa katika serious issues. Please please pleeeeeease.....
 
Siasa?😳😳😳 How? Ben Saanane ni Binadamu anatafutwa sababu ni binadamu wewe unasema siasa?why? Uwe serious.jamaa kasema pasipo kuweka siasa.kasema atafutwe ben saa nane we unasema analeta siasa?
Kama anataka taarifa za Ben Saanane kwanini asiende kuuliza kituo cha Police kwa maana wao ndio wana dhamana ya usalama wa raia na mali zao@
 
Mkuu, acha kuleta masuala ya kisiasa katika serious issues. Please please pleeeeeease.....
Mi nilidhani hiyo technologia ni kuwatafuta waliopotea katika mazingira tatanishi, anyway ni uzi wako endelea kujadili
 
Angesema atafutwe mwakipesile ungesema analeta ukabila? Angesema atafutwe abdallah ungesema analeta udini? Unataka aseme atafutwe nani? Mr Smith?
Huyo jamaa yako ameuliza swali lake on the wrong place and at the wrong time. Ila ameomba radhi na mimi nimekwisha msamehe
 
sawa mkuu@
Yaani hawa wahusika wote wawili nawafahamu... na ni kweli Kupaza alikuwa bwana shamba ambaye alihusika pia na uchinjaji wa wanyama kabla ya kuwa mwalimu wa lugha ya Kiswahili kwa wazungu. Mwivano dah!!
 
Na hii kitu ndo naisikia leo alooo ilikuwa hatari
 
ni kweli Kupaza alikuwa bwana shamba ambaye alihusika pia na uchinjaji wa wanyama kabla ya kuwa mwalimu wa lugha ya Kiswahili kwa wazungu. Mwivano dah!!
Sahihi. Pole kaka mkubwa ninaona umeandika kwa hisia sana
 
  • Thanks
Reactions: Mj1
Back
Top Bottom