Polio Vaccines hamna nchi nzima?

Polio Vaccines hamna nchi nzima?

Karucee

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2012
Posts
18,155
Reaction score
34,303
Wadau habarini za jioni. Mie naombeni kuuliza manake nashindwa kuelewa eti chanjo za polio hamna nchi nzima?

Mtoto wangu alipokuwa na wiki moja alipokea shot ya BCG na Polio drops. Ila hakupata pale nilikojifungulia. Ni spitali private so ikabidi twende Mwananyamala na namshukuru Mungu tulipata. Sasa basi the next one ni akiwa na mwezi mmoja na nimezunguka sana wanasema ni spitali zote nchini.

Nimebahatika kupata pale Premier Care Namanga kwa shilingi elfu kumi. Naomba kama kuna mtu anafahamu atueleze what is going on na wapi zinapatikana sababu sio wote wanauwezo huo wa kulipia chanjo.
 
Dah lakini ARVs fake zipo!!!!! Kweli hata hiyo basics za watoto hakuna!!! EPI ipo na inafanya nini?
 
Hii nchi sijui inaelekea wapi. Na mhusika anapata usingizi kabisa???
 
Ni kweli hata mimi jana nilikosa matone ya polio,mwanangu ana mwezi sasa.Nimeambiwa hakuna tz nzima eti..inashangaza!
 
Ni kweli hata mimi jana nilikosa matone ya polio,mwanangu ana mwezi sasa.Nimeambiwa hakuna tz nzima eti..inashangaza!
Wiki iliyopita mimi nilimpeleka mtoto hapo Neema hospital iliyopo Kimara stopover na akapewa matone,sasa sijajua wiki hii kama bado wanayo
 
Back
Top Bottom