Wadau habarini za jioni. Mie naombeni kuuliza manake nashindwa kuelewa eti chanjo za polio hamna nchi nzima?
Mtoto wangu alipokuwa na wiki moja alipokea shot ya BCG na Polio drops. Ila hakupata pale nilikojifungulia. Ni spitali private so ikabidi twende Mwananyamala na namshukuru Mungu tulipata. Sasa basi the next one ni akiwa na mwezi mmoja na nimezunguka sana wanasema ni spitali zote nchini.
Nimebahatika kupata pale Premier Care Namanga kwa shilingi elfu kumi. Naomba kama kuna mtu anafahamu atueleze what is going on na wapi zinapatikana sababu sio wote wanauwezo huo wa kulipia chanjo.