The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Umati wa maofisa wa polisi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wamekacha na kujiunga na kundi la waasi la M23, huku wakijisajili kwa ajili ya kupatiwa mafunzo ya kijeshi na waasi hao.
Reuters imeripoti jana kuwa askari hao waliovalia sare za kijeshi za rangi ya bluu walionekana wakiimba na kupiga makofi katika mji wa Bukavu uliotekwa na M23 Jumamosi Februari 16,2025.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Muungano wa Waasi wa Alliance Fleuve Congo (AFC/M23), Lawrence Kanyuka, takriban maofisa wa polisi 1,800 wamejisalimisha huku wakijisajili kwa ajili ya kupatiwa mafunzo na wengine 500 wakifanya hivyo siku moja baadaye.
Askari hao wanajiandaa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo mapya chini ya mamlaka ya waasi hao (M23) ambao wanadaiwa kuungwa mkono na Serikali ya Rwanda, japo Rais Paul Kagame kukanusha madai hayo.