Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Askari polisi wa Kituo cha Kibaya wilayani Kiteto Mkoa wa Manyara, Geogre Mwakambonjo (40) amefariki dunia baada ya kugongwa na lori alipokuwa amepanda kwenye pikipiki.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ahmed Makarani amesema tukio hilo limetokea leo Jumanne Desemba 24 mwaka 2024.
Kamanda Makarani ameeleza kuwa askari polisi huyo amefariki dunia baada ya kugongwa na lori akiwa amepakizwa kwenye pikipiki.
Ameeleza kuwa, askari polisi huyo, amepata ajali hiyo eneo la Msasani, Kata ya Maisaka mjini Babati kwenye barabara kuu ya Arusha - Dodoma.
Kamanda Makarani amesema chanzo cha kifo cha askari huyo ni uzembe wa dereva aliyekuwa anaendesha lori kwa kutokuwa makini.