Polisi akatwa panga akikamata mtuhumiwa

Polisi akatwa panga akikamata mtuhumiwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
polisi-pic.jpg

Polisi mkoani Kilimanjaro, wanamsaka mtuhumiwa wa mauaji aliyemjeruhi kwa kumkata kwa panga kichwani, askari wa jeshi hilo, wakati askari huyo na wenzake walipofika nyumbani kwake kwa lengo la kumkamata.

Askari huyo wa kituo cha Polisi Sanyajuu wilayani hapa, Wilfred Kavishe (pichani) alijeruhiwa kichwani usiku wa Septemba 27 na mtuhumiwa huyo, ambaye ni miongoni mwa watuhumiwa wa mauaji yaliyotokea kijiji cha Naibili.

Siku hiyo, baadhi ya wananchi wa kijiji hicho walimshambulia kwa mapanga mtu aitwaye Serafini Mrama na kufariki dunia wakimtuhumu kumkata ng’ombe wa jirani yake mguu wa nyuma na kuondoka nao kwa ajili ya kitoweo.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Yahaya Mdogo, alipoulizwa jana na Mwananchi, alithibitisha kutokea kwa tukio la askari huyu kukatwa kwa panga kichwani na kwamba taarifa za kina zitatolewa kesho na kamanda wa Polisi Mkoa, Simon Maigwa.

“Ni kweli hilo tukio lipo na tuna masikitiko makubwa kuwa kijana wetu amejeruhiwa akitekeleza majukumu halali na ya kisheria na walifuata taratibu zote. Njoo Jumatatu (kesho) afande RPC (Maigwa) atakupa taarifa kamili,” alisema.

Madai ya bomu la machozi
Kaimu kamanda huyo alisema Kamanda Maigwa ndiye anayeweza kutolea ufafanuzi wa taarifa za matumizi ya bomu la machozi katika purukushani hizo ambalo inadaiwa lilisababisha uharibifu na kumlazimisha mtuhumiwa kutoka ndani.

Wakati Kaimu kamanda huyo akisema hayo, gazeti hili lilimtafuta askari huyo ambaye alieleza siku hiyo saa 5 usiku walikwenda kumkamata mtuhumiwa, lakini walipofika nyumbani kwa mtuhumiwa, alijifungia ndani na kugoma kutoka.

“Sasa katika kufungua ule mlango ndio alitoa panga na kunikata kichwani ila baada ya muda nyumba ilianza kutoka moshi alitoka na kukimbia ila mke wake alitoka salama,” alisema polisi huyo bila kufafanua moshi huo ulisababishwa na nini.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Naibili, Sebastian Shirima ambaye ana undugu na mtuhumiwa wa shambulizi hilo, alieleza siku hiyo usiku saa 6 alijulishwa kuwa polisi na viongozi wa vijiji, wamefika nyumbani kwa ndugu yake.

Katika mawasiliano hayo, alijulishwa askari hao walikuwa wameambatana na mtendaji wa kijiji hicho pamoja na mwenyekiti wa kijiji. “Ni kweli polisi walifika wakiongozana na viongozi wa kijiji; huyu ndugu yangu naambiwa akamkata kwa panga polisi na katika purukushani hizo kulisikika milio kama wa bomu la machozi lililorushwa ndani ya nyumba,” alidai Mallya.

Mtendaji wa kijiji hicho, Melikiao Patrick, alieleza siku hiyo saa 2 usiku alipigiwa simu na polisi muda wa saa mbili usiku kwamba wanakwenda kijijini kwake kwa ajili ya kuwatafuta washukiwa kadhaa wa tuhuma za mauaji.

“Baada ya hapo tuliongozana hadi katika nyumba ya mtuhumiwa ambapo tulijitambulisha na kumtaka afungue mlango hakufungua ndipo askari alisukuma mlango akakatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na damu nyingi kutoka”alidai.

Mtendaji hiyo alidai baada ya kuona damu, yeye alikimbilia kwenye gari ya polisi na baadaye ilibainika kuwa mtuhumiwa huyo alifanikiwa kutoroka na hivyo Jeshi la Polisi kuanzisha msako mkali likishirikiana na kijiji kumsaka mtuhumiwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Jamaa ana kesi mbili nzito namuona akifia mahabusu kabla ya hukumu
Gazeti la mwamanchi limekuwa la udaku,kwani hawajii kuwa Nyumba yote imeteketea kwa moto,na mke wa mwwnye nyumba waleenda nae polisi baadaye wakamuachia kienyeji bila kuandika maelezo,

Kwani hawajii IGP amepeleka Timu ya uchunguzi?
 
Ss hapo police wakijibu mapigo kwa wahalifu kuna watu wanapiga kelele wafate sheria.
Je mtu kama uyo kwa kitendo icho mbona wale watetea wahalifu awajaanzisha nyuzi zao
 
Unaendaje kumkamata mtu saa tano usiku kwake? Kashagoma kufungua akihofia usalama wake iweje mvunje mlango maana huwezi sukuma mlango uliofungwa ukafunguka alichokipata polisi ni halali yake huna waranti ya ukaguzi ukiingia ni kosa mpka uwe na kibali na mjumbe sasa polisi ya bongo hawawezi hayo mambo wacha agugumie maumivu ya panga na mwamba hawampati hata kidogo sio mjinga yeye
 
Ss hapo police wakijibu mapigo kwa wahalifu kuna watu wanapiga kelele wafate sheria.
Je mtu kama uyo kwa kitendo icho mbona wale watetea wahalifu awajaanzisha nyuzi zao
Tulia wewe afande kufia kazin hio sio shida ndio kaz yenyewe hio
 
Unaendaje kumkamata mtu saa tano usiku kwake? Kashagoma kufungua akihofia usalama wake iweje mvunje mlango maana huwezi sukuma mlango uliofungwa ukafunguka alichokipata polisi ni halali yake huna waranti ya ukaguzi ukiingia ni kosa mpka uwe na kibali na mjumbe sasa polisi ya bongo hawawezi hayo mambo wacha agugumie maumivu ya panga na mwamba hawampati hata kidogo sio mjinga yeye
Mbona hapo taratibu zote zilifuatwa?, Huyo jamaa kwa vyovyote ni muhalifu sugu wa kitongoji hicho, mtu ambaye siyo sugu hawezi kufanya hivyo kumkata askari kwa panga bila hofu, atafutwe aozee ndani kama sabaya!
Kumbuka polisi hufanya kazi kwa saa 24.
 
Back
Top Bottom