Polisi aliyekamatwa asema walipewa maagizo kumtia adabu Ojwang'

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
KONSTABO James Mukhwana, ambaye kwa sasa anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya kikatili ya mwanablogu na mwalimu Albert Ojwang’, hatimaye amevunja ukimya na kufichua kwa kina kilichotokea usiku wa Juni 7, 2025, akiwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi

Maelezo ya kina, ambayo Citizen TV imeyapata kwa kipekee, yanaweka wazi mambo mapya kuhusu tukio hilo la kusikitisha ambapo Ojwang’ alipoteza maisha akiwa mikononi mwa polisi

Katika taarifa hiyo ya kushtua iliyorekodiwa na Konstebo James Mukhwana kwa maafisa wa Mamlaka ya Uangalizi wa Polisi (IPOA), jina la Mkuu wa Kituo (OCS), Samson Talaam, linatajwa moja kwa moja, akidaiwa kutoa amri ya “kumuadhibu” Ojwang’amri ambazo Mukhwana anadai zilitoka kwa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Eliud Lagat.

Haya yanakuja huku OCS Talaam akiwa tayari amekanusha hadharani kuhusika na tuhuma hizo za mauaji.

Katika maelezo yake kwa wachunguzi wa IPOA, Mukhwana anasimulia jinsi alivyoitwa ofisini kwa OCS usiku huo akiwa kazini. Alielezwa: “Kuna agizo kutoka kwa DIG Lagat. Unamfahamu? Kuna maafisa kutoka makao makuu ya DCI wanamleta mtuhumiwa hapa saa mbili usiku. Waambie wale wafungwa wamuonyeshe adabu kidogo.”

Soma pia: Mtaalamu aliyevuruga mfumo wa CCTV kwenye kituo cha polisi alichoshikiliwa Ojwang' kwa malipo ya Ksh 3,000 amekamatwa

Mukhwana anasema alipokuwa na mashaka kuhusu hatari ya agizo hilo, aliambiwa wazi kwamba yeye ni afisa mdogo na kutakiwa asihoji maagizo, vinginevyo angekumbwa na madhara.

Majira ya saa tatu usiku, gari aina ya Subaru nyeusi liliwasili kituoni, likiwa na mtu aliyefungwa pingu, ambaye baadaye alithibitishwa kuwa ni Albert Ojwang’. Mukhwana anasema alimwita OCS Talaam, ambaye alithibitisha kuwa huyo ndiye mtuhumiwa aliyekuwa anazungumziwa.

Ojwang’ alifungiwa rasmi saa tatu na dakika ishirini usiku, na muda mfupi baada ya hapo mateso yakaanza kwenye selo ya mwisho karibu na vyoo. Mukhwana anasema wafungwa wanne—Collins Ireri, Gil Ammiton, Brian Mwaniki na Erick Ndambuki—waliagizwa kumshambulia. Wote hao wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Mateso yalipozidi, Mukhwana anadai kuwa yeye na afisa mwingine, PC Kimani, walikimbilia katika selo hiyo kujaribu kuzuia mateso hayo. Ojwang’ alikutwa akiwa anatokwa na damu na akiwa amesimama kwa taabu akiegemea ukuta, Mukhwana anasema alimuomba Naibu OCS, Samuel Nganga, ampeleke Ojwang’ hospitalini mara moja
===

Police Constable James Mukhwana, currently in custody over the brutal killing of blogger and teacher Albert Ojwang’, has broken his silence, revealing chilling details about what transpired on the night of June 7, 2025, while Ojwang’ was held at the Central Police Station.

A blow-by-blow account, exclusively in Citizen TV’s possession, now sheds new light on the events of that night when Ojwang’ died while in custody.

The damning statement, recorded by detained Police Constable James Mukhwana, directly implicates the Officer Commanding Station (OCS), Samson Talaam, alleging that he issued instructions to “discipline” Ojwang’—orders Mukhwana claims originated from Deputy Inspector General of Police Eliud Lagat.

This comes despite OCS Talaam having publicly distanced himself from the murder allegations.

In his detailed statement to investigators from the Independent Policing Oversight Authority (IPOA), Mukhwana narrates being summoned to the OCS’s office during his shift. He was allegedly told: “There is a directive from DIG Lagat. Do you know him? There are officers from the DCI headquarters bringing a suspect here at 8:00 p.m. Tell the inmates to discipline him a bit.”

When Mukhwana raised concerns about what could go wrong, he says he was warned against questioning orders as a junior officer and bluntly told that disobedience could cost him.

Later that night, at around 9:00 p.m., a black Subaru pulled up at the station. Inside was a man in handcuffs, later identified as Albert Ojwang’. Mukhwana says he called OCS Talaam, who confirmed that Ojwang’ was the suspect in question.

Ojwang’ was booked into custody at around 9:20 p.m., and shortly after, the assault began inside the last cell opposite the toilets. Mukhwana states that four inmates—Collins Ireri, Gil Ammiton, Brian Mwaniki, and Erick Ndambuki—were instructed to carry out the beatings. All four have since been arrested and arraigned in court.

As the beatings escalated, Mukhwana claims he and another officer, PC Kimani, rushed in to stop the torture. Ojwang’ was found bleeding, leaning against the wall. Mukhwana says he immediately asked the Deputy OCS, Samuel Nganga, to take Ojwang’ to hospital





​
Source: CITIZEN DIGITAL




​
 
Hata IGP wa kwetu TZ kuhusu account yake kuna mtu kashazikwa huku.

Huyo mkuu wa polisi aliye toa order alikuwa na ukwasi ambao mpaka kanunua majumba dubai.
Na ndio aliyekuwa anahusika na mauwaji ya Gen z.

Hii ishu ruto anazidi kujikaangaa.
 
Walikuja hapa kwetu kutushika sharubu tukawaacha. Huko kwao wanakijua wanachokipata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…