LGE2024 Polisi: Aliyekuwa mgombea wa CHADEMA hakutekwa, alijificha ili asigombee nafasi ya Uenyekiti wa Mtaa

LGE2024 Polisi: Aliyekuwa mgombea wa CHADEMA hakutekwa, alijificha ili asigombee nafasi ya Uenyekiti wa Mtaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia na kumhoji aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Uenyekiti katika mtaa wa Buswelu A kupitia CHADEMA, Pastory Apolinary Sililo anayedaiwa kuwa alitekwa na watu wasiojulikana.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa amesema mnano tarehe 26 mwezi huu, mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Victoria, Ezekia Wenje alionekana kwenye vyombo vya habari akitoa taarifa ya kutoweka kwa mgombea huyo, huku akidai alitoweka katika mazingira ya kutatanisha na kwamba ametekwa na maisha yake yapo hatarini na kuliomba Jeshi la Polisi kumtafuta mgombea huyo.

Pia soma: LGE2024 - Mgombea CHADEMA adaiwa kutekwa Polisi kuingia mzigoni kuanza kufuatilia

Kamanda Mutafungwa amesema kabla Wenje hajatoa taarifa hiyo tayari tukio hilo lilikuwa limesharipotiwa katika kituo cha Polisi Buswelu kwamba mgombea huyo hajulikani alipo, na upelelezi ulianza mara moja kwa kuwahoji watu mbalimbali akiwemo mke wake.

Aidha, Kamanda Mutafungwa amesema walipomhoji afisa mtendaji wa mtaa wa Buswelu A, Godso Mkama alisema mgombea huyo hajatekwa ambapo alieleza kuwa mgombea huyo alimwambia kuwa hawezi kugombea tena na kwamba anajiondoa kwenye mchakato na kusema ataondoka kwenye mtaa huo hadi mchakato wa uchaguzi utakapokamilika ndipo akaenda kujificha mtaa wa Buhila A, wilayani Ilemela kwa ndugu yake aitwaye Zaituni Selemani Misonge anapodaiwa kujificha tangu Novemba 25 hadi alipokamatwa na Polisi.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Kamanda Mutafungwa amesema baada ya kukamatwa amekanusha kutekwa na kusema alijificha ili kukwepa kugombea nafasi hiyo ya uenyekiti, mbali na mgombea huyo pia Jeshi la Polisi linawashikilia ndugu zake, Zaituni Selemani Misonge na Aneth Joshua Bumale.
 
Polisi wanaajiriwa kwa
Urefu
Mbio
Siyo akili, huwezi kuwa kamanda wa mkoa bila kuwa na kadi ya chama
Tukumbuke ya zerote Stephen. Baadae mtotow ake akaja kuwa DED Handeni sijui bado yupo au la!
 
Malipo ni hapa hapa duniani. Maaskari mnatumika kuwabeba CCM. Halafu CCM wao wao wanakula pensheni zao mpaka wanazimaliza 🤣🤣🤣 maaskari wakistaafu hawapati pensheni zao wanakuta 0. Wanaishia kulalamika na kuishi maisha magumu. CCM kuleni pensheni zao mpaka ziwe 0 🤣🤣
Huyu mwingine alikuja JF kulalamika



 
Back
Top Bottom