Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Katika Kijiji cha Kaunda eneo la Navakholo kaunti ya Kakamega, Polisi Patrick Nyapara wa utawala amemuua mkewe, Christine Maonga (28) kwa kumpiga risasi mara tatu kichwani baada kuzozana kwa muda mrefu.
Patrick alidai kuwa mkewe alipata ujazito nje ya ndoa na kumsingizia kuwa yeye ndiye baba wa mtoto huyo baada ya kujifungua
Inadaiwa kuwa ndoa ya wawili hao imekuwa ikikumbwa na changamoto nyingi sana tangu mwanamke huyo alipojifungua mtoto wao wa kwanza na ilibainika kuwa mwanaume huyo alikuwa akimtishia mkewe hata katika mitandao ya kijamii
Afisa huyo alitoweka baada ya kutenda kitendo hicho huku mwili wa marehemu ukipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti mjini kakamega
Marehemu alikuwa mwalimu katika shule ya upili ya Navakholo