Polisi apandishwa kizimbani baada ya kunaswa na meno ya tembo yenye thamani ya tsh. Milioni 121.5...

Polisi apandishwa kizimbani baada ya kunaswa na meno ya tembo yenye thamani ya tsh. Milioni 121.5...

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Askari wa Jeshi la Polisi, Ramadhan Selemani (27), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shitaka la kukutwa na meno ya tembo yenye thamani ya Sh. Milioni 121.5.

1.jpg


Mbali na Selemani, mshitakiwa mwingine katika kesi hiyo ni raia ambaye anatambulika kwa jina la Hamis Mwanya (22), ambao walifikishwa jana mahakamani hapo mbele ya Hakimu Nyigulila Mwanseba.

Wakili wa Serikali, Mwanaisha Komba, alidai mbele ya Hakimu Mwanseba kuwa Julai 19, mwaka huu katika eneo la Tazara wiliyani Temeke, jijini Dar es Salaam, washitakiwa hao walikutwa na nyara za serikali

ambazo ni meno ya tembo manne pamoja na vipande 12 vya meno hayo vilivyo na thamani ya Sh. milioni 121.5, ambayo ni mali ya Serikali.

Hata hivyo, washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi isipokuwa Mahakama Kuu na pia upelelezi wa shauri hilo haujakamilika.

Hakimu Mwanseba aliahirisha shauri hilo hadi Agosti 7, mwaka huu, na washitakiwa walirudihswa rumande.





POLISI APANDISHWA KIZIMBANI BAADA YA KUNASWA NA MENO YA TEMBO YENYE THAMANI YA TSH. MILIONI 121.5....!! - GUMZO LA JIJI
 
Angalia majina ya watuhumiwa vs majina ya mwendesha mashtaka na hakimu
 
Back
Top Bottom