Wana JF heri ya mwaka mpya. Kuna suala nimelisia sasa naomba kuelimishwa sheria inasemaje.
Kuna ndugu mmoja kanunua gari kwa mtu. Siku moja akasimamishwa barabarani akaambiwa gari lake inadeni la tzs 150,000/- akaoneshwa jina la dereva na lesseni namba ya huyo dereva. Pia, akajulishwa makosa yaliyotendwa.
Makosa matatu, yalitendwa kwa nyakati na mazingira tofauti.
Huyu mmiliki mpya wa gari akajitetea kwamba makosa yale hakuyatenda yeye na gari lilikuwa chini ya miliki ya mtu mwingine. Tafiki polisi aliyemkamata hakumwelewa. Akadai aachiwe leseni. Leseni itarudishwa deni likisha lipwa. Leseni imeshikiliwa na huyo trafiki kwa zaidi ya mwezi.
Je! Ni halali kosa la dereva wa gari kulipishwa faini ya dereva mwingine?
Je! Ni halali kwa afisa wa trafiki kushikilia leseni ya mtu asiyena kosa lo lote?
Sent using Jamii Forums mobile app