Polisi auwa mkewe kwa risasi na kujiuwa

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253

Askari Polisi Stephen Mungai Kinuthia wa jimbo la Nakuru nchini Kenya, amemuuwa mkewe kwa kumpiga risasi kichwani na kisha kujiua mwenyewe mbele ya mtoto wao ambaye alishuhudia tukio zima.

Kinuthia ambaye alikuwa skari polisi wa kituo cha Molo, amempiga risasi mpenzi wake huyo mara tatu kwa kutumia bunduki ya AK47 wakiwa nyumbani kwao.

Shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mlinzi wa eneo hilo amesema walisikia kelele za watu wakilumbana, na walipokuwa wakikimbilia kujua kulikoni walisikia milio ya risasi na kisha kukawa na ukimya.

Majirani wa eneo hilo wamesema walisikia kelele za mtoto akilia kwa sauti huku akisema baba anamuuwa mama.

OCPD wa Nakuru Joshua Omukatta amesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo, huku miili ya marehemu wote ikiwa imepelekwa katika hospitali ya serikali ya Nakuru.

Chanzo: EATV
 
Hapo chanzo cha mauaji ni papuchi na michepuko hakuna ubishi
 
maafande bhana hahahhahaha marumbano kidogo risasi. duuuuh
 
dogo wamemuathiri kisaikolojia maisha yake yote
 
Aisee huenda aligundia sio mwanae yule,

Ila maamuzi mabaya sana yale
 
Mtoto kama ni wa kiume atachukia kazi ya polisi na kama ni wa kike atachukia kuolewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…