Polisi: Bastola ya Nape Nnauye iliyoibwa nyumbani kwake Kawe Beach imepatikana mkoani Mbeya

Polisi: Bastola ya Nape Nnauye iliyoibwa nyumbani kwake Kawe Beach imepatikana mkoani Mbeya

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam imesema silaha ya mbunge wa Mtama mkoani Lindi iliyoibiwa kupitia dirishani nyumbani kwake Kawe beach jijini Dar es salaam imepatikana.

Silaha hiyo aina ya bastola ikiwa na risasi 14 imepatikana mkoani Mbeya baada ya ushirikiano wa polisi wa mikoa hiyo miwili na mtu mmoja anashikiliwa kuhusiana na tukio hilo.

Chanzo: Ayo tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Kuna watu ni wazembe aisee! Yaani silaha unaiweka sehemu ya wazi, tena dirishani kiasi cha mwizi kuichukua tu kwa urahisi na kutembea nayo!!

Halafu huyu Nape si ni Mbunge wa Mtama huyu!! Sasa huko Kawe kwa Halima Mdee anafanya nini tena!! Badala ya kurudi Jimboni kwake! yeye anakula tu bata Mjini!!!
 
Mh...
Mkuu,polisi waliuliwa kabisa na bunduki zikabebwa
Sijui uliwapa jina gani na ulichukuliaje tukio?
 
Bongo watu sio violent hata mwenye bastola akikabwa anajiuliza Kwanza hawa wanataka kunikaba huku akiendelea kujiuliza anakabwa kweli huku akiwa na siraha...ngoja niendelee kutengeneza picha Kama kweli siraha iliibiwa dirishani...
 
Back
Top Bottom