Nimecheka sana, tuna Askari wa ajabu sana sana.
Waliruhusu gari bovu likazunguka kote likaenda kuungulia Chato baada ya vitisho vya Wasira na uvccm.
Such a pathetic statement!
Waliruhusu gari bovu likazunguka kote likaenda kuungulia Chato baada ya vitisho vya Wasira na uvccm.
Such a pathetic statement!
- Tunachokijua
- Jeshi la Polisi Mkoani Geita linaendelea kuchunguza kufanya uchunguzi wa Tukio la kuchomwa kwa Gari T.658 DQL liliokuwa likitumika kufanyia Matangazo ya Mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana wilayani Chato Mkoani Geita.
Akithibitisha tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita ACP Adam Maro amesema mpaka sasa chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na wametuma Askari kwa ajili ya kwenda kchunguza tukio hilo.
"Ilipofika saa nane usiku (kuamkia Agosti 2, 2023) mlinzi anayeitwa Cyprian akawa anapiga kelele anasema kuna moto kwenye gari. Watu wote wakatoka wakawa wanakabiliana na moto ule, wakafanikiwa kuuzima"
ACP Maro amefafanua kuwa hadi sasa, Agosti 2, 2023, chanzo cha moto huo hakijajulikana na Idara ya zima moto bado inafuatilia kisha taarifa itatolewa.
Mlinzi wa hoteli ilipokuwa imepakiwa gari hiyo anashikiliwa na Jeshi kwa ajilli ya uchunguzi. Aidha, kitengo cha Upelelezi kipo mtaani kikifuatilia tukio hilo.
Gari hiyo inatajwa kupata madhara kwenye kioo na tairi ya nyuma upande wa kushoto pamoja na jenereta.
Akimalizia maelezo yake, ACP Maro amesema;
"Ni mapema mno kusema chanzo cha moto ni nini, au ni mapema sana kusema pengine kuna sabotage sababu eneo lenyewe ni eneno le ye uzio. Tuache kwanza tuendelee kufanya upelelezi mwisho wa siku chanzo cha moto kitajulikana."
JamiiForums imejiridhisha kuwa kuwa hadi Agosti 3, 2023, Polisi ilikuwa haijatoa maelezo mengine yoyote ya ziada, ikiwemo yale yanayohusisha madai ya kuwa gari la CHADEMA likukuwa bovu.
Aidha, Madai haya yanayotajwa kuchapishwa na Kurasa za mitandao ya Kijamii ya East Africa TV hayapatikani kwenye kurasa hizo.
Agosti 2, 2023, Makamu Mwenyekiti CHADEMA, Tundu Lissu alikuwa ziarani Chato ambapo alifanya mikutano ya hadhara pamoja na kuzuiwa na Umoja Vijana wa CCM waliotoa taarifa kuwa hawataruhusu akanyage hata hatua moja akiwa huko.