Polisi chunguzeni ukweli kuhusu tukio la watoto watatu wa familia moja kufa kwa kuungua moto Rombo, Kilimanjaro

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Ni taarifa nimeisoma kwa majonzi sana juu watoto watatu wa familia moja, Erick (9), Joshua (7) na Gidion Theodory (2) kufa kwa kuungua moto ndani ya nyumba na mama yao kudai kwamba waliungua kwa moto uliosababishwa na wao kuchezea kibatari wakati yeye akiongea na simu na mume wake nje ya nyumba yao.

Haiingii akilini kwamba huyu mama, Karesma Theodory (39), akiwa anaongea na simu nje ya nyumba, hakuweza kusikia kelele za watoto wake hadi moto ulipokuwa mkubwa wa kushindwa kuingia ndani kuwaokoa.

Kwanini utoke nje ya nyumba kwa kuongea tu na simu, tena na mume wako mwenyewe?

Hapa inawezekana kabisa huyu mama alikuwa amewafungia watoto ndani ya nyumba na yeye kwenda kwenye mishe mishe, na hata kwenye kunywa pombe. Polisi fanyieni uchunguzi tukio hili, kwanza ni saa ngapi alikuwa akiongea na simu, na pia kama mnaweza kuona alikuwa wapi akiwa anaongea na simu, kama ni kweli.

Angalieni kama kwenye eneo la nyumba hiyo kuna signal ya kutosha kuongea na simu hata ukiwa ndani ya nyumba, na muulizeni kwanini alitoka nje ya nyumba basi kuongea na simu kama signal inapatikana hata akiwa ndani ya nyumba.

Mambo kama haya ya uzembe katika kulea na kuangalia watoto yanatia hasira hadi mtu unatamani kuwepo na sheria ya watu wanaozembea kulea watoto wahasiwe.
---

Watoto watatu familia moja walivyoteketea kwa moto Rombo
Ni tukio linaloweza kudumu katika kumbukumbu ya maisha ya Karesma Theodory (39) wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro, baada ya kushuhudia watoto wake watatu wakiteketea kwa moto.

“Nilisikia watoto wakiniita, mama mama huku moto ukiwa umeshika kasi,” alisimulia Karesma ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Lessoroma wilayani Rombo na kueleza namna alivyojitoa mhanga kuwaokoa wanawe pasipo mafanikio.

Tukio hilo lililoibua simanzi, lilitokea usiku wa kuamkia juzi kijijini humo kwa kile kinachodaiwa chanzo ni kibatari ambacho watoto walikuwa wakikichezea ndani ya nyumba yao.

Watoto hao waliofariki dunia kwa kuteketea kwa moto wakati mama yao akiwa ametoka nje akiongea na simu na mume anayeishi nchini Kenya ni Erick (9), Joshua (7) na Gidion Theodory (2).

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema chanzo cha moto ni kibatari ambacho watoto hao walikuwa wakikichezea ndani wakati mama yao akiwa nje.

“Ni kweli hili tukio limetokea jana (juzi) usiku, lakini chanzo chake ni kibatari walichokuwa wakikichezea hawa watoto, mama yao akiwa hayupo, kwa hiyo hiki kibatari kilidondoka kisha nyumba kushika moto,” alisema Kanali Maiga.

Mtendaji wa Kijiji cha Lessoroma, Emma Mosha alisema tukio hilo limewashtua na kuwashangaza wengi na kusema kuondokewa na watoto watatu wote kwa mpigo sio jambo jepesi.

“Kwa kweli hili tukio limeniumiza sana, ni tukio gumu, yaani halivumiliki, kuondokewa na watoto watatu na wamekufa kifo cha mateso sio kitu cha kawaida, kwa kweli limetuumiza sana,” alisema Emma.

Mmoja wa majirani, Atanasi Joseph, alisema: “Yaani kwa kweli hatujui tuseme nini, maana hili tukio ni gumu, kuondokewa na watoto kwa wakati mmoja ni pagumu kidogo, cha msingi tunamwombea huyu mama uvumilivu maana sio kitu rahisi.”

Miili ya watoto hao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Kituo cha Afya cha Karume kilichopo wilayani humo kwa ajili ya taratibu za maziko.

Mama asimulia
Akielezea tukio hilo lilivyotokea, Karesma alisema alitoka nje na kuwaacha watoto wake hao wakiwa chumbani na yeye akaenda kuongea na simu na mume wake anayeishi Kenya.

Alisema wakati amesimama alisikia sauti ya watoto ikiita, “mama mama,” alipogeuka aliona moto unawaka kwenye nyumba yake na kurudi mbio ili kwenda kuwaokoa watoto waliokuwepo ndani.

“Nilikuwa nimetoka nje kuongea na simu ya wifi yangu, nikawa nimesogea hadi kichumini. Nilikuwa nimewaacha watoto wangu ndani, wakati nasema nimpe wifi yangu simu yake nikasikia kelele,” alisema.

Karesma alisema moto huo ulikuwa unawaka sebuleni huku watoto wakiwa chumbani, alipambana kuwaokoa kwa kuvunja mlango wa chumbani lakini alishindwa baada ya moto kumpiga machoni na sehemu ya mkononi.

“Nilijaribu kuvunja chumba walichokuwa wanangu nikashindwa maana niliishiwa nguvu, nilishindwa kupiga hata ukunga kutokana na zile sauti za wanangu,” alisema.

Mwanasaikolojia Josephine Tesha wa jijini Dar es Salaam alisema mtu anapopatwa na tukio la aina hiyo anatakiwa aachwe aomboleze kwa hali yake ya asili bila kuzuiwa ili yale machungu yaondoke, kumzuia inaweza kumletea madhara.

“Huyu mama amepitia kipindi kigumu sana kwa tukio lilivyo. Mtu wa aina hii unatakiwa umpe hadi miezi sita ili amalize ule uchungu kiasili kabisa usimzuie. Baada ya huo muda ni vizuri akaonana na mwanasaikolojia.”

Alisema kama asipopatiwa ushauri nasaha uchungu unaweza kumsumbua kipindi kirefu cha maisha yake na hili linazuilika tu kwa kumuwahi na kumpatia ushauri nasaha.

Source: Watoto watatu familia moja walivyoteketea kwa moto Rombo
 
Hao wazazi tayari wamepata adhabu ya uzembe.
 
Dah Mungu awalaze mahali pema watoto wa taifa letu.
Uzembe wa mzazi ndio umekuwa chanzo cha vifo vyao.
 
Kwa sasa tuondoe neno "uzembe" hakujua kama yangetokea. Angeziba kibatari kabla ya kuondoka? Poleni sana wafiwa, hiyo ni ajali tu! Pumzikeni kwa amani watoto wetu. Mmekufa kwa mateso.
 
huo uchunguzi utasaidia nini watoto waisha kufa mamayao kakosa kuwahurumia polisi ndio watakao weza kuwahurumia
 
Safaricom netwk inasumbua kwl ukiwa ndan uwez ongea Kuna sehemu netwk inapatkna ndo wengi hukusanyika kuongea
 
huo uchunguzi utasaidia nini watoto waisha kufa mamayao kakosa kuwahurumia polisi ndio watakao weza kuwahurumia
Kwani mtu akifa uchunguzi unafanywa wa nini wakati huyo mtu alishakufa? Wakimaliza uchunguzi kuhusu sababu ya kufa kwake atafufuka?
 
Mchezo huo moto uwake akiwa nje ashindwe kuwatoa?
 
huo uchunguzi utasaidia nini watoto waisha kufa mamayao kakosa kuwahurumia polisi ndio watakao weza kuwahurumia
Ingekua watu wote wana mawazo kama yako basi ajali zisingekua zinafanyiwa uchunguzi,Ndege zinaanguka na kuungua moto ila lazima kuwe na crash investigation,

Mtu hata akijinyonga au kunywa sumu,lazima kuwe na uchunguzi.
 
Back
Top Bottom