Polisi: David Djumbe amepatikana, tunachunguza waliomkamata Bunju

Haki ya kuishi kwa amani bila uwoga wa kutekwa Tanganyika imekuwa bidhaa adimu!
 
Wamenichekesha eti wametaja gari na jina za mmiliki ila watekaji hakuna hata mmoja anaejulikana jamaa wanatuona sisi ni viazi sana..
 
Nikisema kuwa polisi hawana akili siwatukani bali utoto walioonyesha kwenye sakata la Jumbe unathibitisha kauli yangu. Afisa wa polisi aliyeongea na Golugwa alisema kuwa wamemfuata Jumbe hapo Chadema HQ kwa vile ametoroka akiwa chini ya ulinzi hii ikimaanisha kuwa wanajua nani walimkamata na kumuweka chini ya ulinzi, sasa wanapokuja na madai ya kuchunguza nani waliomkata hiki ni kichekesha na kutaka kuwafanya Watanzania wote ni wajinga kama walivyo wao Polisi. Acheni Mungu aitwe Mungu, yaani wamepigwa upofu hadi wanaitangazia dunia kuwa wao ndiyo huteka watu na kuwaua kisha kupoteza maiti zao halafu wanakuja na utetezi kuwa watu wanajipoteza sababu ya mapenzi au kukimbia madeni. Za mwizi ni arobaini na jana ndiyo zimetimia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…