Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Jeshi hilo, wamechangia damu kwa ajili ya kuwasaidia wananchi pindi wanapopata Changamoto za uhitaji wa damu katika Wilaya ya Mbogwe Mkoa wa Geita.
Kamishna Msaidizi wa Polisi ACPMagai Chassa amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limetumia maadhimisho hayo kuikumbuka benki ya damu salama ambapo wamechangia damu kwa ajili ya benki hiyo pia kufanya matembezi ya hiari kwa kushirikiana na Wananchi kwa lengo la kufikisha ujumbe kuhusiana na masuala ya uhalifu.
ACP Chassa ameendelea kufafanua kuwa kilele cha maadhimisho hayo kitaifa kitakua Septemba 17 mwaka huu huko Mkoani Kilimanjaro ambapo kwa mkoa wa Geita walikutana na makundi mbalimbali ikiwemo wanafunzi, bodaboda, nyumba za ibada na vyombo vya habari kwa ajili ya kutoa elimu juu ya wananchi kujiepusha na vitendo vya uhalifu.
Maadhimisho hayo yanaenda na kauli mbiu ‘’Huduma Bora za Kipolisi kwa Umma zinapatikana kwa kubadilika kifikra, Usimamizi wa Sheria na Matumizi ya TEHEMA’.