Elly B
JF-Expert Member
- Jan 11, 2011
- 1,194
- 906
Binafsi, kama ilivyo kwa wananchi wengi wa nchi hii, naendelea kusikitishwa na tabia ya Polisi kutumiwa na Serikali kwa maslahi ya CCM. Tabia hii siyo tu inawakosesha wengine haki, bali inafanya wananchi wakose Imani na uadilifu wa Polisi ilinayotakiwa kulinda usalama wa raia na mali zao (siyo chama na mali zake).
Siku za karibuni kumeibuka tabia ya ajabu ya watu kubambikiwa kesi kwa maslahi ya chama tawala au wakati mwingine kwa lengo la kuficha aibu ya kushindwa kazi yao.
Tumeona jinsi kesi ya utekaji wa Dr.Ulimboka ilivyokuwa na mafinyufinyu ya aina yake tangu kukamatwa kwa Mulundi kule Kawe. Kwa mtu wa kawaida kabisa ilikuwa ni ngumu kuanza kuamini acha kuelewa, kuwa mtu atatoka Kenya na kujua Mabwepande iko wapi, kwa Ulimboka ni wapi, anatumia namba gani na anatembela viwanja gani. Na hasa atoke kwao kuja kumteka Dr. Ulimboka kwa baya lipi alilowatendea Wakenya? Ni wazi kama nilivyowahi kusema siku za nyuma hii ilikuwa ni njia ya kuwapumbaza wananchi wa nchi hii, ambao wamezoeleka kwa kusahau haraka mara baada ya kuzuka jambo jipya. Kwa hiyo wana imani sasa wameshasahau kila kitu! Hata baada ya mahakama kuthibitisha kuwa Mulundi Joshua hana hatia bado Polisi haioni aibu kwa tabia yake ya ajabu! Ni vema ikakumbukwa kulikuwa na tume ya IGP ambayo mpaka leo haijatoa majibu kama ilivyoahidiwa. Mimi nadhani ni muda muafaka kwa polisi kuwaambia wananchi ni nani alimteka Dr.Ulimboka kama Mulundi hana hatia. Vinginevyo Wananchi hawataona ni uwongo kuwa serikali ina mkono katika zoezi lile. Vinginevyo ni kwa nini hiyo tume au hata CID wasimhoji Dr. Ulimboka mpaka leo?
Halafu kuna hili la Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri, Absalom Kibanda kutekwa na kuumizwa vibaya. Kuna ushahidi wa kuonyesha kuna mkono wa dola hata nyuma ya zoezi lile kwani Absalom alishapata kutahadharishwa mapema na alikuwa tayari kutoa ushirikiano. Mbona hatuoni maendeleo ya lolote? Ni kweli polisi ya Tanzania ni hopeless kiasi cha kushindwa kumpata hata mhalifu mmoja wa hayo matukio?
Siku za hivi karibuni kumekuja hili la Ugaidi! Ni ajabu kuwa kila anayekamatwa anatoka mahabusu na kulalamikia kuteswa huku akilazimishwa kukubali kuwa Mwenyekiti, Katibu au wengineo katika CHADEMA ni Waratibu wa mipango ya ugaidi. Wengine utasikia wanasema hadharani walikamatwa na makosa mengine na kuunganishwa na kesi za ugaidi eti kwa sababu una namba ya mtu wa CHADEMA! Kesi zote zikipelekwa mahakamani zinafutwa kwa kutokidhi vigezo vya Ugaidi. Hivi ni kweli ofisi ya DPP na DCI zimeshindwa kubaini ukweli wa mashtaka au kuna shinikizo nyuma ya hayo mahsitaka? Ni kweli DPP ameshindwa kuelewa sheria kiasi cha kushindwa kupambanua ni kesi ipi ni ya jinai na ipi ni ya Ugaidi? Siamini hilo. Ninachoona ni muendelezo tu wa tabia ya kubebeshana kesi feki.
Na kuna hii tabia ya aibu kabisa iliyozaliwa siku hizi ya polisi kumkamata mtuhumiwa, kumpiga mpaka kumwua na kutelekeza maiti bila hata kuwataarifu ndugu zake. Hivi ni nani aliyesema ukiwa polisi unakuwa siyo binadamu tena?
Labda ni kweli huyo ni mhalifu, lakini ni kwa nini asifikishwe mahakamani ahukumiwe kwa sheria kuliko kumpa hukumu bila kuzingatia uzito wa kosa wala sheria? kuna tofauti gani sasa kati ya polisi wanaoua watuhumiwa na raia wanaoua wahalifu bila kuwapeleka kwenye vyombo husika? Hii ni aibu kwa jeshi la polisi.
Ni wazi wanaobambikwa kesi ni wengi kuliko tunavyoweza kusikia kwani siyo wote wamepata nafasi ya kutoka mahabusu, Siyo wengi wanapata dhamana na ni wachache wanaoweza kushauriwa na mawakili.
Kinachonistua ni hii hali ninayoona ya kuwa wote walotekwa na wote walibambikwa kesi wana mwelekeo mmoja wa kukosoa seriakli aidha kwa magazeti yao na vyombo vya habari au kwenye majukwaa ya siasa, jambo ambalo linafanya niamini kuwa hakuna la ziada zaidi ya serikali kutumia polisi kunyamazisha upinzani, kudumaza demokrasia na kuzuia huru wa kupashana habari. Nilitegemea katika jamii ya watu wastaarabu ,mtu anapotoa tuhuma atatakiwa azithibitishe. akishindwa mahakama ziko wazi. Hii tunayofanya ni tabia ya kuonea aibu kwani si ya kibinadamu na haiendani na jinsi jumuiya ya kimataifa inavyotuchukulia.
Na labda mimi ndiyo nakosea kufikiria au uelewa wangu ni mdogo. Basi ni kwa nini Polisi isikanushe tuhuma zote kuwa haihusiki na hayo?
Nimalizie na kuwakumbusha polisi kuwa wana wajibu wa kuwatumikia wananchi. Siyo vyama vya siasa. Na hapa ninamaanisha hawapaswi kitumikia CCM leo, wala chama chochote kesho, kwani kwa kufanya hivyo polisi inachagua kuwabagua wengine na hii ni kuvunja katiba na haki za wasi wa vyama hivyo na za wasio na vyama kabisa. Na haina tija sana kwani hakuna chama kitakachotawala milele ingawa Wananchi watakuwepo milele! Kwa hiyo kitu pekee polisi inaweza kufanya kurudisha imani ya wanachi iliyopotea ni kuacha kutumika kwa mslahi ya kisiasa. Polisi ifanye kazi ya ulinzi kama inavyotegemewa. Iache vyama vya siasa vifanye siasa. Polisi iwe wazi kuwa imezidiwa na haina uwezo wa kupambana na wahalifu badala ya kuwadanganya wanachi waliwaajiri na wanowalipa mishahara kwa kodi za jasho lao, kwa kuwabambika kesi watu wengine ili wananchi waridhike ilihali siyo kweli. Hii ni aibu kwa jeshi la polisi na kukosa uadilifu kwa kiwango kikubwa. Na kwa mtindo huu wa sasa polisi itegemee nini kutoka kwa wananchi?