Polisi, Jeshi na vyombo vya Usalama Tanzania mjiepushe na Ujinga Huu

Polisi, Jeshi na vyombo vya Usalama Tanzania mjiepushe na Ujinga Huu

kibogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
9,739
Reaction score
4,742
Tarehe 21.9.2013 kulipotokea lile tukio la uvamizi pale Westgate Kenya tumeshuhudia Askari wakiingia katika katika ile vita huku wakiwa hawana kinga yeyote ya kuzuia Risasi za wale magaidi na kwa mtazamo wangu nahisi wengi wa askari waliokufa katika vita ile ni hao ambao hawakuwa na kinga, Ombi langu kwa Askari,JWTZ na vyombo vingine vya usalama tunapoingia katika uokoaji na mashambulizi kama yale iwapo yatatokea hapa kwetu (siombi na naomba mungu aepushie mbali) basi tujikinge ili kuepusha maafa kwa askari wetu kwani hawa magaidi walikuwa hawaangalii aliye na uniform au asiye na uniform wote walikuwa ni Target kwao.

kenya 4.PNG

kenya 1.PNG

kenya_westgate_shootings_029.jpg

kenya 11.PNG

Hii ni mifano michache ya askari wa Kenya ambao hawakuvaa kinga yeyote kuzuia vichwa vyao ambavyo kama tulivyoshuhudia hawa Al Shabab wao walikuwa wanalenga vichwa tu.
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Mkuu katika post zoote kuhusu tukio hili, hii nimeipenda. Sijui taaluma ya mtumaji lakini ukweli kwenye vita ya kisasa, burret proof ni muhimu mno. Kuanzia juu, kichani HELMET mpaka mwilini. Asante sana na bila shaka wahusika wamekusikia.
 
Wanazidiwa hata na vodafaster!!
 
Mkuu katika post zoote kuhusu tukio hili, hii nimeipenda. Sijui taaluma ya mtumaji lakini ukweli kwenye vita ya kisasa, burret proof ni muhimu mno. Kuanzia juu, kichani HELMET mpaka mwilini. Asante sana na bila shaka wahusika wamekusikia.

Na pia usisahau bomu halichagui hata uvae chuma yatakuhusu tu
 
Wamekusikia walengwa mkuu endelea kutoa elimu ya uraia lakini ulipaswa ujue kwanza gharama ya vifaa hivyo ili ujue kama inawezekana askari wote wanaokwenda kwenye mapambano kama wanawaze kupatiwa wote.
 
Kama wapiganaji wangekuwa ndiyo viongozi wa jeshi , ungeeleweka , hivi unajua kwanini hospitali za Tanzania haziboreshwi ( huwa zinapakwa rangi tu ) ? Ni kwa sababu viongozi wenu hawatibiwi nchi hii .
 
Kiusalama bullet proof vest inatakiwa ivaliwe ndani hii isimpe adui wasaa wa kukulenga maeneo mengine iwapo akijua umevaa vest hasa iwapo ukiwa unapambana na majamaa ambao wako trained kama AL SHABAB ambao wana shabaha...

bullet proof inavaliwa kwa nje iwapo unaenda kupambana na vibaka-majambazi ambao wamevamia duka wao silaha wanafyatua tu wana aim mtu ila hii mijamaa ya al shabab hai aim wana aim kiungo... aidha kichwa, kifua au tumbo
 
bora hata Field force wetu,ambao muda wote wako proof bullet ukitaka ukweli nenda kwenye mikutano ya siasa au wale wa tuktuk ambao wako doria mitaa mbalimbali dsm
 
It is a good advice, we saw it in Afghanistan, US forces uses them but for snipers, bullet proof is nothing! remember there were very few movement in there, and the enemy was stationary and strategically positioned so could spot and choose where to shoot.
 
Wakenya wlaikumbwa na vigugumizi vingi sana kwenye hili tukio, nadhani hata hawakuwa na uhakika whether watumie wanajeshi au polisi.
 
Back
Top Bottom