Nyamesocho
JF-Expert Member
- May 5, 2023
- 487
- 1,287
Najitokeza hapa kulalamikia usafirishaji wa bangi unaofanywa na vijana wa boda boda licha ya kwamba ni kinyume kusafirisha lakini imekuwa hatari kwa wakazi na wanafunzi wanaotumia hii barabara inayosafirisha bangi.
Barabara ya Kijiji cha Nyamwigura kupitia vijiji vya Magoma, Nyasaricho, kitagasembe, Gwitiryo, Sirari, wakazi na wanaotumia wapo kwenye risky kubwa kwa ajali za barabarani.
Hawa wasafirishaji bangi wataua watu kwenye hii barabara kwa sababu speed wanayopita kwenye hiyo barabara ni ya hatari sana. Nyakati za jioni watoto wanakuwa wanatoka shule, inakuwa ni hatari sana kwa usalama wa watoto, mpaka wazazi wanakuwa na wasi wasi usalama wa watoto na watu wengine na hao hao boda boda wasafirishaji.
Je, Jeshi la Polisi Tarime Rorya mnasubiri watu wafe ndio mchukue hatua kwenye hii barabara?
Tunalitaka Jeshi la Polisi kudhibiti hili, bora wasafirishe usiku kuliko mchana, maisha ya jamii ya maeneo haya yapo hatarini, kila siku jioni wanafunzi, watumia barabara wanaponea chupuchupu kugongwa na wasafirishaji bangi.