mchuku wa mangi
Member
- Jun 25, 2022
- 12
- 8
Kuna waimbaji wanaimba 'mwenye pea' si mwenzako ni kweli mwenye pesa si mwenzako,wengine wanasema mwenye nguvu mpishe, huwezi shindana naye.
Nimeonelea nianze kuhathisia kisa hiki kwa kuanza hivyo pengine huko mbele mtanielewa namaanisha nini?
Mwezi novemba 2019 eneo la Majengo mjini Moshi karibu kabisa na ofisi za kikosi cha zimamoto na uokoja, maisha ya Kijana Richard Emmanuel Pusindare akiwa umri wa miaka 20 maisha yake yalibadirika ghafla baada ya kugongwa na gari la mke wa mmiliki wa gereji Kubwa kabisa mjini Moshi ya DAG ama Dura Auto Garage.
Kiana huyo alikuwa anatokea eneo la Mbuyuni kuelekea Majengo alipofika eneo hilo karibu na mafundi selemara gafla gari liliingia barabarani kutokea upande wake wa kushoto pasipo kuchukua tahadhari na hivyo kijana huyo kuivaa gari hiyo na hapo ukawa mwanzo wa mateso
Baada ya ajali hiyo kijana huyo alikimbizwa Hospital ya Rufaa ya KCMC ambako alilazwa kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya kuvunjika mguu wake wa kushoto na mpaka anatoka shilingi milioni mbili aliziacha hapo kama gharama za matibabu.
Anakiri kuwa mme wa mwanamke huyo na mmiliki wa Gereji hiyo alichangia sh,550,000 kwenye matibabu hayo na pia katika kuwekewa mguu bandia tajiri huyo alichangia 200,000 katika gharama halisi inayofikia milioni 1.2.
Pamoja na yote haya Jalada la kesi hiyo hadi leo mwaka wa tatu lipo kwenye makabati kwenye kituo cha polisi Majengo, hakuna kilichofanyika na kijana huyo hawezi kupata haki yake ikiwamo fidia ya yale aliyoyapa kutokana na bima ya gari hilo kwa vile polisi 'wameua' kesi .
"Baada ya kupata ajali bba yangu ndo alikuwa anafuatilia na walikutana na DURA lakini baba akasema tusubirie kwanza mimi nitoke hospital ili tukae pamoja tujue cha kufanya ikiwamo namna atakavyonifidia kutokana na hii ajali lakini bahati mbaya baba yangu alifariki dunia",anasema kija huyo.
Pusindare kwa sasa amepata ulemavu wa kudumu ambao haumwezeshi tena kukimbizana na kazi kama ilivyokuwa anaomba msaada wa kisheria kupata haki yake lakini jambo la kwanza ni mshitakiwa wake afikishwe mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.
Kazi kwenu polisi,naomba kuwasilisha