Ila jamani tusipende kukuza mambo. Hawa wanaotekwa ni watu ambao wanajihusisha ma mashirika na mataifa ya nje katika kuikosoa serikali.
Mwisho wa siku kutekwa kwao inakuwa sio ajenda ya kiusalama zaidi bali ni ya kisiasa.
Kuna mataifa kama mexico, watu hutekwa kwaajiri ya pesa au kutekwa kwaajiri ya kubakwa,l au sextrafficking au mauwaji ya visasi na ujangiri wa kijamii.
Mimi hii kitu siwezi kuishadadadikia kwasababu wahusika wanayo option ya kufanya mambo mengine zaidi ya kujihusisha na hizi cheap politics. Maana ni kama ukaishi miji kama Colombia halafu uanze kupiga vita madawa ya kulevya, u wont last a week, utauwawa, the way to be safe ni kukeep out of the way.
Tunao uhuru wa kuhoji na kuiuliza serikali maswali. Ila hatuna uhuru wa kupika majungu na vijembe kwa kushirikiana na mataifa ya nje na NGO zao. Haya ndio yanayowafanya hawa wahusika kuingia matatizoni.......
Maana hata wale ambao wamejificha ughaibuni nilitaraji kama kuna maovu watayaibua baada ya kupewa siri na wadau wao humu ndani ya nchi ila naona wanapiga vijembe tu..... Ni ndege ikinunuliwa waseme tumepigwa ni ya mtumba, mara waseme sijui nini ambazo ni rubbish tupu.
Hawa wanaharakati walikuwa wapi kipindi cha kikwete, awamu ambayo walarushwa na mafisadi walikuwa na nguvu kuliko awamu yoyote na uhalifu ulikuwa nje nje.....
Leo masilahi yao yamebanwa vinatokea vibwana mdogo kisa vimejua kutype basi vinaanza kuandika andika upuuzi ma cooked up rumors.
So mimi kimsingi hili tatizo la hawa wahusika kutekwa nalitazama kisiasa zaidi na si kiusalama.
Kwa wale msio jua maana ya hatari ya usalama wa raia na utekaji hebu ingieni YouTube uone stories, wanatekwa watoto wadogo wa miaka miwili mitatu, na wanapatikana wameshauwawa.
Wanatekwa mabinti na wanawake wanatoweka na kurejea wameuwawa au wamefanyiwa ukatili wa kijinsia. Wanatekwa watu na miili inapatikana haina viungo vya ndani, wanatekwa watu halafu watekaji wanademand pesa......
Sasa haya matukio ndio yakuweza kufanya taifa lizizime juu ya uovu. Sio huu upuuzi wa kujitakia....
Hata wewe hapo unaesoma, ukitaka kujitafutia matatizo ni rahisi sana, anza kuandika habari za kichochezi ambazo hauna hata ushahidi nazo na uwe busy sana kutumia social media kuhamasisha watu kuziamini, siku si nyingi tutaona post yako, kuwa umepotea umetekwa na watu wasiojulikana.
Stay out of dirty politics.....
Sent using
Jamii Forums mobile app