Polisi Manyara wagundua kiwanda bubu cha kuzalisha pombe kali feki, watumia jina la Konyagi

Polisi Manyara wagundua kiwanda bubu cha kuzalisha pombe kali feki, watumia jina la Konyagi

John Walter

Member
Joined
Aug 14, 2017
Posts
68
Reaction score
63
Jeshi la polisi mkoa wa Manyara katika operesheni zao, wamegundua kiwanda bubu kilichopo Mtaa wa Ngarenaro mjini Babati, kinachozalisha pombe kali feki zinazofungashwa kwenye vifungashio vya kampuni ya Konyagi.

Jeshi hilo limekamata shehena ya pombe hizo feki huku wakiwaweka wafanyakazi wa kiwanda hicho chini ya ulinzi.

Kamanda wa polisi mkoa wa manyara Benjamin Kuzaga akizungumza kwa njia ya simu amesema kuwa operesheni hiyo inalenga kuondoa bidhaa feki ambazo nihatarishi kwa afya ya binadamu na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo.

Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho feki aliejulikana kwa jina babu moses amesikika akisema wanafanya kazi hiyo ili kujiingizia kipato na kwamba wanao usajili ambao hajauweka bayana.

Makamu mwenyekiti viwanda kutoka chama cha wafanyabiashara mkoa wa Manyara (TCCIA) David Mulokozi amesema kuwa uwepo wa viwanda bubu unaikosesha serikali mapato pamoja na kuathiri afya za watumiaji wa bidhaa hizo na kuisababishia serikali hasara kubwa kwa kuwa hawalipi kodi.

Pombe hizo feki zinaonekana zikiwa zimebandikwa stika zenye nembo ya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambapo mtaani zinaingizwa zikiwa na jina la Konyagi.

picha 2.png


Pia soma - Matumizi ya Kemikali ya Ethanol yanaweza kuathiri ini na kusababisha Saratani
 
Ndio kufikiri njee ya box huko, hii ni kesi ya uhujumu uchumi pole sana kwa washukiwa na familia zao
 
Wanaweza kushtakiwa na kampuni ya konyangi kwa kuwaharibia biashara zao
 
Daa! Kweli binadamu sijui umfanye nini? Anachojali ni kipato chake, si usalama wa afya za wengine! Hii ni HATARI sana!
 
konyangi,k-vant na pombe zote bei kuanzia 1500 mpaka elfu 15000.tuna kunywa gongo chafu na pili ukitaka kuharisha ndo hizi pombe
 
Haa Nyagi Feki Hii Ndiyo Inafanya Ukate Moto Haraka
 
KINACHOUMIZA KICHWA HAYO MABOKSI NA HIZO CHUPA ZENYE VIFUNIKO KABISA OG WANAPATA WAPI???
 
Kama formular ya ladha, harufu na alcohol concentration wameipatia basi wanatakiwa wabadili kidogo na wasajili brand yao wawe rasmi
 
Au Huku Ndio Kutafuta Ajira Kwa Kuchangamkia Fursa !!?? Hii Ni Hatari Sana Na Ndio Maana Magonjwa/Matatizo Ya INI Na FIGO Yanazidi Kuongezeka (Pombe Feki, Formalin, Maji Ya Kunywa Feki.....). Wanastahili Kuchukuliwa Hatua Kali Maana Huu Ni Uuwaji.
 
Back
Top Bottom