Polisi Mbeya wamkamata Joseph Ngoya akiwa na noti bandia za Tsh. 10,000
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia JOSEPH NGOYA mwenye umri wa miaka 34, Mkazi wa Mbozi Mkoa wa Songwe kwa tuhuma za kupatikana na Noti bandia za shilingi elfu kumi.
Ni kwamba mnamo tarehe 23.02.2023 huko maeneo ya Kituo cha Mafuta (Sheli) ya Kazibure iliyopo barabara Kuu (Tunduma Road) katika Mji mdogo wa Mbalizi mtuhumiwa alikamatwa akiwa na karatasi 15 alizozikata kwa mfano wa noti ya TSH 10,000/= akiwa katika harakati ya kuziingiza kwenye mzunguko.
Mtuhumiwa amehojiwa amekiri kujihusisha na matukio ya utapeli katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya.