Polisi: Mbowe amepelekwa Dar kwa Mahojiano, atarejeshwa Mwanza

Polisi: Mbowe amepelekwa Dar kwa Mahojiano, atarejeshwa Mwanza

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza imethibitisha kumshikilia Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwa mahojiano.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi amesema kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani nchini alitiwa mbaroni alfajiri ya kuamkia jana Jumatano Julai 21 akiwa hoteli ya Kingdom mtaa wa Ghana alikokifikia.

"Baada ya kumkamata, wenzetu wa Dar es Salaam nao walitueleza kuwa wanamtafuta kwa makosa mengine anayodaiwa kuyafanya huko; hivyo tulimsafirisha kwenda Dar es Salaam anakoendelea kuhojiwa," amesema Kamanda Ng'anzi.

Amesema kiongozi huyo wa Chadema hivi sasa yuko kwenye mikono salama ya polisi Mkoa wa Dar es Salaam na atarejeshwa Mwanza baada ya mahojiano ili aunganishwe na wenzake 15 wanaoshikoliwa kuhusiana na kongamano la Katiba Mpya lililozuiwa na jeshi hilo jana.

Mwananchi
 
Tuwe wavumilivu, unapo fanya chokochoko na fujo kuna majibu yake. Kabla kuwasulubu jirani zako kwa unayoyaona ni makosa, kwanza jiangalie kama wewe uko vizuri na huna dosari.

Tunawasema viongozi wa serekali kuwa wanavunja katiba na tunadai katiba mpya, na tunamuona Mbowe anavyo ikanyaga katiba ya chama na namna anavyo kiendesha chama kwa kidikteta lakini aa hatumuoni wala hatusubutu kumshutumu. Tunaona ni mwamba.

Siasa za kinafiki hazileti maendeleo bali huleta mfarakano.
 
Haya mambo bhana.Ila CHADEMA na nyie mkue kidogo,mbinu za kiharakati kujiimarisha zitakua zinawakuza na kuwapoteza.Kwa alivyo Rais wa sasa, hata nyie mnapaswa kutumia mbinu za kistarabu ambazo haziwaharibii jina.Issue ya katiba CHADEMA wanashindwa kuicheza katiba ni takwa la watu wote wa nchi husika japo huwapo machampioni ili kufanikisha.

Huwezi kudai kATIBA kama vile ni yakwako pekee yako, ili hali unajua kua unahitaji kutumia watu wa mlengo wako na wasio wa mlengo wako kupenyeza ajenda, hisia na malengo yako.

Kwa mwendo huu wa mmoja analazimisha mwingine anagoma lazima mpigane virungu na sisi common soliders hatutajua tumuunge mkono nani maana bado wote hawajatushawishi lipi ni bora kuliko jingine .Kama kumbukumbu zangu ziko sawa katiba mpya ilikwama kwenye muundo wa serikali tatu au mbili, hivyo tungeanzia hapo.Na jambo la serikali sio la kulazimisha ni suala la mwafaka tu bila mwafaka hakuna jema

Labda kama katiba ni gia ya kujiboost vingenevyo ni muhimu kua na njia zilizosahihi kwa wakati sahihi.
 
Back
Top Bottom