Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Katika Operesheni hiyo iliyofanyika Disemba 23, 2024 katika eneo la kizuizi cha Polisi Vamos, Mikumi katika Wilaya ya Kipolisi Ruhembe alikamatwa dereva aitwaye Evodius Faustin Mkembela (37) akiendesha gari namba T.305 CZS / T.185 EHE aina ya BEN BEN akiwa katika hali ya ulevi na alipopimwa alikutwa na ulevi kiasi cha 505.1 mg/100ml.
Pia limemkamata dereva aitwaye Edmund Mugina (38) mfanyabiashara mkazi wa Mbezi kwenye kizuizi cha barabarani akiwa anaendesha gari namba T.187 ELD aina ya Mazda akiwa anatokea Dar-es Salaam- Morogoro akiwa katika hali ya ulevi kiasi cha mg.415.5 mg/1001.
Mwingine ni Dereva Hashim Nasibu Juma (32), aliyekuwa anaendesha gari la abiria T.629 DQE ZHONGTONG mali ya kampuni ya Sweet Africa alikamatwa akiwa amezidisha idadi kubwa ya abiria 7 zaidi ya idadi inayotakiwa kisheria.
Kutokana na makosa hayo, Jeshi la Polisi limewafungia madereva hao leseni zao za udereva kwa mujibu wa kifungu cha 28 (3) (8) cha sheria ya Usalama Barabarani sura ya 168. Uchunguzi zaidi wa shauri lao unaendelea kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Vilevile, msako huo ulifanikisha kukamatwa kwa madereva wengine 45 wakiwa wamefanya makosa ambayo ni hatarishi kwa watumiaji wengine wa Barabara, Makosa hayo ni pamoja na kuzidisha abiria kupita kiasi ambapo madereva 14 wamekamatwa wakiwa wamebeba abiria zaidi ya kiwango kinachokubalika kisheria na madereva wengine 19 wamekamatwa wakiwa na makosa mbalimbali ya usalama barabarani. Aidha madereva 12 wa magari ya mizigo nao wamekamatwa wakiwa wamebeba abiria kwenye magari ya mizigo kinyume na sheria.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa madereva wote na watumiaji wengine wa barabara kuendelea kuheshimu na kufuata sheria, taratibu na kanuni za usalama barabarani ili kulinda maisha na usalama wa watumiaji wote wa barabara. Yeyote atakayekwenda kinyume na sheria za usalama barabarani hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa ikiwemo kuendelea kuwafungia leseni madereva wazembe.
Imetolewa na:
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Morogoro