Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Jeshi la Polisi Tanzania limeeleza kuwa linafanyia uchunguzi madai ya kutekwa kwa Katibu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Mwanza, Amani Manengelo (30).
Inadaiwa kuwa Manengelo alichukuliwa na watu wanne kutoka nyumbani kwa rafiki yake, Jovin Thomas (32), ambaye pia ni Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Misungwi.
Kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Audax Majaliwa, taarifa zinaonyesha kuwa Manengelo alichukuliwa Februari 14, 2025, na tangu wakati huo hakuna yeyote aliyeweza kuthibitisha alipo, ikiwemo ndugu na jamaa zake.
Soma pia: Amani Manengelo, Katibu wa BAVICHA Mkoa wa Mwanza, ameripotiwa kutekwa na kupotea tangu tarehe 14.02.2025 huko Misungwi
SACP Majaliwa ameongeza kuwa uchunguzi bado unaendelea, huku akitoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa zozote zitakazosaidia katika upatikanaji wa Manengelo.