Polisi na ujambazi igunga

Kite Munganga

Platinum Member
Joined
Nov 19, 2006
Posts
1,773
Reaction score
952
Tarehe 15 usiku palitokea ujambazi wa kiaina katika kumbi mbili Igunga ambazo zina Guest House na wateja wakaibiwa fedha nyingi tu na mali zingenezo, sasa mazingaombwe yalianza kesho yake tarehe 16/11/08 ambapo mwaathirika wa ujambazi huo alipomtambua na kutoa taarifa kuwa kati ya majambazi yale mmoja alikuwa ni askari Polisi wa hapo hapo Igunga anayeitwa "Mwaka" ndiye aliyekuwa ameshika Bunduki kwenye tukio siku hiyo, OCS akishirikiana na askari wa upelelezi Manda kwa harakaharaka wakatuma Askari kuanzisha kamatakamata mjini hasa ikilenga wazururaji na wageni na kuwaunganisha na kesi ya ujambazi huo huku wakimwacha askari wao bila kumfungulia mashtaka au kufanya upelelezi kama kweli alihusika au la, Kwa wenyeji wa Igunga wanadai kuwa wanahisi kuwa ujambazi huo ulipangwa na Polisi kwani sio kawaida kabisa Polisi kukosa kufanya doria sehemu hizo siku za week-end na inazidi kutia mashaka kwa hao wazurulaji kupelekwa mahakamani kesho yake tarehe 17 wakidaiwa kuwa ndio waliotenda kosa hilo huku Polisi aliyetajwa akiachwa huru huria mtaani lakini akiwa kasimamishwa kazi, kinachofanywa ni wale vijana wabebe kesi na Polisi isihusishwe kabisa na matukio ya siku hiyo ili kuficha uchafu ulio ndani ya Polisi wetu wa Igunga, mwisho napenda mtu mwenye namba za IGP Mwema au RPC wa Tabora ili nikomae nao, pia si vibaya nikipata namba za wakili yeyote aliyeko Tabora
 

Ndugu nimejaribu kutafuta sijaipata namba ya Mwema lakinikuna hawa makamada wake ingawa kati yao wengine wameshastaafu. wapigie waulizie utapata msaada kuanzia hapo.
Hizi namba ziliwahi kuwekwa hapa katika post fulani na Shy ila ile ya mwisho nimeiongeza mwenyewe si ya Shy.


Hiyo nadhani RA aliitoa bure kwa muungwana. Si unaweza kuona ni special number?
 
Asante mkuu, nimeweza kuingia kwenye website yao na kutuma malalamiko Head office-Dar, pia nimepata namba za RPC Tabora nafikiri nitawasiliana naye, Asante kubwa!!!!
 
Suala la kwanza hapo ni kupigania hao vijana waliokamatwa waachiwe mara moja halafu huyo Mwaka aswekwe ndani mara moja. Hawa Polisi kwanini wanataka kuwashonesha miaka 30 vijana bila makosa?????? Mwema waokoe wanyonge hao, kwani polisi wamekuwa wakilalamikiwa sana kuhusu ubambikizaji kesi kwa vijana wanyonge!!!!!!
 

Makamanda wa polisi Tanzania wanatumia Hotmail, Yahoo, Gmail na Lycos.

Kazi tunayo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…