Polisi na vyama vya Upinzani. Je, Polisi wako Juu ya Sheria?

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Posts
4,786
Reaction score
1,715
1. Utangulizi
Jeshi la Polisi ni chombo cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichoundwa ili kuwahakikishia wananchi usalama wao na mali zao, kudumisha amani na utulivu katika jamii, pia kuzuia, kubaini na kupambana na uhalifu.

2. Lengo la Jeshi la Polisi:
Jeshi la Polisi lipo kwa lengo la kuwahakikishia wananchi usalama wao na mali zao, kudumisha amani na utulivu katika jamii, pia kuzuia, kubaini na kupambana na uhalifu. Jeshi la Polisi lipo kama sheria inavyoelekeza kuhakikisha kuwa kila mtu, wakiwemo askari polisi wanafuata sheria katika kila hatua.

3. Majukumu ya Jeshi la Polisi:
Jeshi la polisi lina kazi kadhaa:

  1. Kuzuia na kudhibiti uhalifu.
  2. Kubaini na kuchunguza vizuri wakati wowote uhalifu unapotokea.
  3. Kutayarisha shauri la kweli na lenye ushahidi ili mwendesha mashtaka aweze kuwasiliana mahakamani.
  4. Kukusanya taarifa kuhusu matukio katika jamii ili kuweza kutimiza jukumu la kudumisha sheria na utilivu.

4 Sheria inayoongoza shuguli za Jeshi la Polisi:
Shughuli za jeshi la polisi zinaongozwa na sheria mbalimbali, lakini kwa kiasi kikubwa:

  1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.
  2. Sheria ya Jeshi la Polisi namba 322 (Police and Auxiliary Services Act 2002 Cap 322).
  3. Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
  4. Kanuni za Polisi (Police General orders).
​
Kwa hiyo Jeshi la polisi lina mamlaka ya kisheria na linapaswa kutumia mamlaka hayo kulingana na taratibu zilizoainishwa katika sheria husika.

Polisi wanaweza kukamata, kufanya upekuzi, kushikilia, kumpeleleza mtuhumiwa, kumhoji shahidi, kufanya mahojiano na mtuhumiwa, kutawanya waandamanaji wenye nia ovu na kuhakikisha usalama wa jamii. Wanapaswa kufanya hivyo kwa kufuata taratibu na sheria na sio vinginevyo. Polisi hawawezi kufanya wapendavyo.
Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai inaeleza njia ambazo polisi na mahakama wanapaswa kufuata katika kuwashughulikia wahalifu. Hii ni pamoja na mamlaka ya polisi na taratibu wanazotakiwa polisi wazifuate. Mfano mmojawapo ni matumizi ya nguvu ya polisi pale anapomkamata mtuhumiwa na nguvu za polisi anapofanya uchunguzi
Sheria ya ushahidi inaeleza kwa undani kinachokubalika mahakamani kama ushahidi. Ushahidi wowote uliopatikana kwa kutumia nguvu, hauwezi kutumika kama ushahidi halali, ikibainika mahakamani kuwa ulipatikana kwa njia batili.
Sheria ya Polisi inaeleza kuhusu uendeshaji wake, nidhamu mamlaka na kazi za polisi na mambo mengine yanayolihusu jeshi la polisi. Sheria hii inasisitiza polisi kutenda haki katika utendaji wao ili kutoa mfano wa kulinda sheria na kanuni za nchi.

Matumizi yoyote mabaya ya mamlaka au uzembe katika kazi ni utovu wa nidhamu na uhalifu. Afisa wa polisi anayetenda hayo anapaswa kuchukuliwa hatua stahiki.

5. Gharama za Shughuli za Polisi
Shuguli zote za polisi zinalipwa na walipa kodi wa Tanzania.

Kila mwaka katika kikao cha bajeti, hutengwa fungu maalum kwa ajili ya uwezeshaji wa utoaji wa huduma za polisi katika jamii. Fedha hizi hupitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa jukumu la ulinzi na usalama wa raia ni suala la muungano. Kitengo cha mipango cha jeshi la polisi huandaa mapendekezo ya bajeti, ambayo hupelekwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi kwa ajili ya kuridhia, kasha hupelekwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi tayari kwa kupelekwa bungeni. Wabunge hujadili na kupitisha bajeti ya polisi. Sehemu kubwa ya bajeti huenda kwenye mishahara. Matumizi mengine ni mafunzo, upelelezi, miundombinu, ujenzi na ukarabati wa nyumba n.k.

Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali hufanya ukaguzi wa akaunti na fedha zilizotumiwa na jeshi la polisi kila mwaka, na taarifa za ukaguzi huwasilishwa bungeni

6. Askari Polisi yuko juu ya sheria?
Hakuna mtu aliye juu ya sheria. Watanzania wote wakubwa kwa wadogo, tajiri kwa maskini, wanaume kwa wanawake, bila kujali dini na itikadi, hata wafanyakazi wa serikali na polisi wanatakiwa kutii sheria na kuishi kwa mujibu wa sheria zilizowekwa nchini mwetu chini ya Katiba yetu.

Hii ina maana kila tendo linalofanywa na askari polisi lifanywe kulingana na sheria, na iwapo polisi hawatafanya hivyo watawajibika mbele ya sheria. Matarajio ni kuwa pia sheria zilizotungwa zimezingatia haki na usawa.

Askari anayevunja sheira anapaswa kuadhibiwa. Tena kwa kuwa polisi amepewa dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sheria, adhabu yake inatakiwa iwe kali zaidi anapovunja sheria.

Iwapo askari ametenda kosa la jinai anapelekwa mahakamani na kuhukumiwa kama mtu mwingine. Lakini anaweza kupelekwa mahakama

7. Polisi na Rushwa:
Jina zuri la Jeshi la polisi na sifa njema ya watumishi wake inategemea sana uadilifu na uaminifu wa kila askari polisi. Kila tendo la rushwa au tuhuma za rushwa dhidi ya askari polisi inatoa sifa mbaya kwa jeshi la polisi. Hivyo, kila polisi anayefahamu kuwa polisi mwenzake anajihusisha na vitendo vya rushwa na akashidwa kuchukua hatua yoyoyte atakuwa anafanya makosa na atahusishwa kushiriki.

8. Polisi na Maandamano na Mikutano ya hadhara:
Mtanzania yoyote ana haki ya kushiriki katika maandamano kwa mujibu wa Ibara ya 20 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ibara hii inatoa haki kwa kila mtanzania kushiriki katika mikusanyiko/maandamano ya amani.

Hata hivyo kundi linalofanya mkusanyiko/maandamano hayo katika maeneo ya wazi linapaswa kutoa taarifa kwa polisi si chini ya saa 48 kabla ya mkusanyiko/maandamano hayo. Taarifa inatolewa kwa kiongozi wa polisi wa eneo ambalo mkusanyiko unapendekezwa kufanyika.

Iwapo kiongozi wa polisi anayepokea taarifa hiyo ana sababu ya msingi ya kuona kuwa mkutano unaopendekezwa unaweza kusababisha uvunjifu wa amani na usalama wa umma anaweza kuzuia mkutano huo kufanyika.

Kwa upande mmoja askari polisi wana wajibu wa kuhakikisha amani inakuwepo. Kwa upande mwingine wanapaswa kuwawezesha wananchi kutumia haki yao ya msingi ya kufanya mikutano ya hadhara kwa amani na utulivu.

Matumizi ya Nguvu dhidi ya Maandamano au Mkutano wa hadhara.
Polisi hawapo kwa ajili ya kuwaadhibu watu, bali kwa ajili ya kuhakikisha kuwa watu wapo salama na sheria hazivunjwi.

Inapotokea kuwa polisi wanalazimika kudhibiti mkusanyiko wa watu, wanapaswa wahakikishe kuwa kila wakifanyacho wanatumia kiasi. Watalazimika kutumia nguvu kama suluhisho la mwisho baada ya hatua nyingine zote kushindikana. Hata hivyo, iwapo nguvu italazimika kutumika basi iwe ya kadiri na inayoendana na mazingira, na itumike kwa muda mfupi iwezekanavyo.

9. Matumizi ya Silaha za Moto dhidi ya Raia.
Kama ilivyosemwa hapo juu, polisi watatumia nguvu kubwa pale ambapo imelazimika tu, na ambapo njia nyingine zote za udhibiti zimejaribiwa na kushindikana.

Polisi anaweza kutumia bunduki katika mazingira yafuatayo:

  1. Dhidi ya mtu anayetoroka, au
  2. Dhidi ya mtu anayefanya jaribio la kutoroka toka kizuizini au
  3. Dhidi ya mtu anayefanya jaribio la kutoroka asikamatwe
  4. Dhidi ya mtu anayetumia nguvu kumwondoa mtu mwingine kutoka kizuizi halali
  5. Dhidi ya mtu anayetumia nguvu kuzuia ukamatwaji halali wa mtu mwingine.
  6. Dhidi ya kundi linaloharibu mali au kutishia usalama wa raia baada ya kuonya mara tatu

Lakini pale tu askari anapokuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hawezi kuzuia utoro huo kwa njia nyingine ana ametoa onyo kwa mtu huyo kuwa bunduki itatumika iwapo hatatii na mtu huyo hajali onyo lililotolewa. Pia endapo polisi watakuwa na sababu ya kuamini kuwa wao wenyewe wako hatarini kuumizwa vibaya.

Wanapolazimika kutumia bunduki dhidi ya kundi linalofanya uharibifu au kutishia usalama wa raia, risasi zinapaswa kulengwa chini na katika kundi linaloonekana ni tishio, lakini si kwa lengo la kusababisha mauaji bali kuwatawanya. Mara kundi linapoonyesha dalili la kutawanyika askari wanapaswa kusitisha upigaji risasi.

Polisi wanaolazimika kutumia risasi wanawajibika kutolea maelezo kila risasi waliyotumia kwa kuandika taarifa inayowekwa katika kumbukumbu.

Pale itakapothibitika kuwa polisi ametumia nguvu isiyohitajika atachukuliwa hatua za kinidhamu au kufunguliwa mashtaka kwa kosa la jinai.

10. Haki za Watu wanaowekwa Mahabusu.
Askari polisi wanawajibika kuwapeleka mahakamani watu waliowaweka mahabusu ndani ya masaa 24. Hata hivyo kwa watu waliokamatwa kwa kibali, kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifo, polisi lazima wakupeleke mahakamani mapema iwezekanavyo.

Askari hawaruhusiwi kupiga, kutisha au kutia hofu mtu aliyewekwa kizuizini, na anayekiuka anaweza kuadhibiwa kwa kosa hilo.

Askari polisi ana haki ya kuhoji walio kizuizini, lakini hawezi kulazimisha mtu yeyote kuongea kitu chochote ambacho mtuhumiwa hana habari nacho, au kitu ambacho mtu hataki kukisema, au kukiri makosa ambayo polisi wanataka akiri.

Ungamo la kosa mbele ya polisi kwa namna yoyote ile halitakubalika mahakamani kama ushahidi.
 
Lwakatare alikaa zaidi ya wiki kabla ya kupelekwa mahakamani.
 
Matumizi ya Nguvu dhidi ya Raia.
Polisi hawapo kwa ajili ya kuwaadhibu watu, bali kwa ajili ya kuhakikisha kuwa watu wapo salama na sheria hazivunjwi.

Inapotokea kuwa polisi wanalazimika kudhibiti mkusanyiko wa watu, wanapaswa wahakikishe kuwa kila wakifanyacho wanatumia kiasi. Watalazimika kutumia nguvu kama suluhisho la mwisho baada ya hatua nyingine zote kushindikana. Hata hivyo, iwapo nguvu italazimika kutumika basi iwe ya kadiri na inayoendana na mazingira, na itumike kwa muda mfupi iwezekanavyo.
Huyu Pinda au hajui sheria au kwa makusudi ameamua kutanguliza chama badala ya maslahi makubwa ya taifa.

Huko tunakoelekea ni lazima tukubali kurudi kwenye utawala wa sheria. Muhimu sana.
 
Pinda anazijua sana sheria sema tu ameamua kujivika uzuzu kwa ajili ya kukitetea chama chake kinachokufa.
 
Naam, ndizo tabia za kipumbavu za kiongozi asiye na hekima...kumbuka mpumbavu kuitwa mpumbavu ni tusi zito kwa wapumbavu!
 
Polisi iko hapa ilipo kwa sababu ya elimu duni, ukosefu wa mafunzo yanayoenda na wakati na pia upungufu wa vitendea kazi.

Polisi wengi bado wanaishi kwenye zama za uongozi wa kiimla, na ikichukuliwa kuwa wengi wao wako kwenye nafasi walizozipata kwa sababu polisi ilikuwa na inaendelea kuwa ni sehemu ambayo vijana wengi wanakimbilia baada ya elimu ya juu kuwashinda (form four and six failure), huku wengi wao ndani ya jeshi wakiwa wamegushi vyeti. Hata hao ambao wana vyeti vya juu kama stashahada (degree) basi zinakuwa pasi zake niza chini kabisa au hazina wigo mpana wa ajira nchini.

Polisi hawajazinduka na kupata ufahamu kuwa nchi kwa sasa inaendeshwa na utawala wa sheria ambapo wananchi wake wengi kwa sasa wanafahamu haki na wajibu wao katika nchi.

Tanzania ya sasa, It's not just about law, what's matter now is a technical aspect of law. Hata kesi nyingi kwa sasa nchini zinachambuliwa na kunyambulishwa kwa njia hii.

Polisi ni taasisi ambayo utendaji wake wa kila siku siyo kwamba tu unatakiwa uendane na sheria bali pia lazima wafahamu jinsi ya kuruka viunzi vya sheria technically. Siamini kama mwenye vyeti vya kughushi, form four au form six failure anaweza kuruka viunzi kama hivi kwa sasa.

Polisi ya Tanzania inahitaji OVERHAUL ili kupambana na challenge za karne ya 21 ambazo ni pamoja na kujua sheria na viunzi vya sheria technically.
 
Ulichoeleza katika bandiko lako upo sahihi kwa asilimia 100,kuwa hivyo ndivyo inavyotakiwa jeshi letu la polisi linavyotakiwa kutekeleza wajibu wake.

Hata hivyo katika kipindi hiki cha awamu ya nne ya utawala wa JK,tumeshuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za ubinadamu unaofanywa na jeshi letu la polisi,ambao haujawahi kufanywa na jeshi lolote la polisi,tokea nchi yetu ipate uhuru.

Mifano ipo mingi ya utendaji mbovu sana wa jeshi letu la polisi,lakini nitajaribu kuitaja michache kuipa nguvu hoja yangu.

Ubambikiaji kesi watuhumiwa,imekuwa jambo la kawaida sana kwa jeshi la polisi.Mfano halisi ni mashitaka ya ugaidi aliyofunguliwa nayo Lwakatare.

Jeshi la polisi pia limekuwa likitumia risasi za moto katika mikusanyiko ya watu pasipo lazima,hadi kusababisha vifo,kama ilivyotokea kwa uchache kifo cha yule muuza magazeti,Ali Zona pale Morogoro na mwandishi Daudi Mwangosi,kule Iringa.

Hata hivyo umeuliza swali la msingi sana kuwa,sasa inapotokea jeshi la polisi,linaendesha shughuli zake,kwa kukiuka sheria za nchi,je jeshi la polisi,je jeshi hilo lipo juu ya sheria?

Jibu hapa liko wazi kabisa ni HAPANA kwa herufi kubwa kabisa.

Lakini pia tujiulize swali la msingi kabisa ni kwa vipi watendaji wa jeshi la polisi,hata pale inapothinitika kabisa bila shaka yoyote,kuwa watendaji hao wameboronga,ni kwa nini basi,hawawajibiki au hawawajibishwi nayule aliyewateua?

Jibu hapa lipo wazi,ingawa katika kikao cha mkutano mkuu wa CCM,aliwaambia wanaCCM,kuwa waache kulitumia jeshi la polisi kuibeba CCM,lakini katika uhalisia,hiyoilikuwa miongoni ya kauli za unafiki wa kupindukia,zilizowahi kutolewa na JK.

Nitaithibitisha kauli yangu,kama kweli JK,alikuwa anatoa kauli hiyo toka moyoni mwake,ilikuwaje akampandisha cheo Kamanda Kamuhanda,badala ya kumfukuza kazi na kumfukuza kazi,baada ya kuthibitika bila mashaka yoyote,kuwa yeye ndiye aliyewaamuru wale askari wake kumlipua Mwangosi,hadi kusababisha kifo chake?!

Kwa maana hiyo hakuna shaka yeyote kuwa JK akiwa ndiye amiri jeshi mkuu wa majeshi yote hapa nchini,na akiwa ndiye mwenyekitiwa chama chake tawala,ndiye kinara wa kuliagiza jeshi lake la polisi,litumie mbinuzozote,hata zile haramu,kuidhibiti CDM,kwa vile tayari TISS,weshawapa taarifa mabosi wao wa CCM,kuwa kwa kasi ya mwendo wa CDM,wanayokwenda nayo kwa sasa, kwa CCM kuishinda CDM,kwenye uchaguzi wa 2015,nafasi hiyo ni finyu kuliko ngamia kupenya kwenye tundu la sindano!!

Kwa hiyo juhudi kubwa inayofanywa na jeshi la polisi kuiokoa CCM,haina tofauti ya madaktari mabingwa wanaokizunguka kitanda cha mgonjwa mahututi ili kuokoa maisha ya mgonjwa huyo,lakini hatimaye mgonjwa huyo anakata roho!!

Ni hakika kabisa bila mashaka yoyote kuwa kwa vituko hivi vinavyofanywa na CCM na mshirika wao mkubwa jeshi la polisi,ni hakika kabisa,kifo cha CCM,kimekaribia sana!!
 
Polisi iko hapa ilipo kwa sababu ya elimu duni, ukosefu wa mafunzo yanayoenda na wakati na pia upungufu wa vitendea kazi.

Polisi wengi bado wanaishi kwenye zama za uongozi wa kiimla, na ikichukuliwa kuwa wengi wao wako kwenye nafasi walizozipata kwa sababu polisi ilikuwa na inaendelea kuwa ni sehemu ambayo vijana wengi wanakimbilia baada ya elimu ya juu kuwashinda (form four and six failure), huku wengi wao ndani ya jeshi wakiwa wamegushi vyeti. Hata hao ambao wana vyeti vya juu kama stashahada (degree) basi zinakuwa pasi zake niza chini kabisa au hazina wigo mpana wa ajira nchini.

Polisi hawajazinduka na kupata ufahamu kuwa nchi kwa sasa inaendeshwa na utawala wa sheria ambapo wananchi wake wengi kwa sasa wanafahamu haki na wajibu wao katika nchi.

Tanzania ya sasa, It's not just about law, what's matter now is a technical aspect of law. Hata kesi nyingi kwa sasa nchini zinachambuliwa na kunyambulishwa kwa njia hii.

Polisi ni taasisi ambayo utendaji wake wa kila siku siyo kwamba tu unatakiwa uendane na sheria bali pia lazima wafahamu jinsi ya kuruka viunzi vya sheria technically. Siamini kama mwenye vyeti vya kughushi, form four au form six failure anaweza kuruka viunzi kama hivi kwa sasa.

Polisi ya Tanzania inahitaji OVERHAUL ili kupambana na challenge za karne ya 21 ambazo ni pamoja na kujua sheria na viunzi vya sheria technically.
Mkuu, kwani Amiri Jeshi mkuu hana sauti juu ya mwenendo huo wa jeshi la polisi?

Je Amiri Jeshi Mkuu anaona kama polisi wanakiuka majukumu yao, au anafurahia kuona wanatenda wanayotenda kwa maslahi ya chama chake?

Kwa nini askari polisi HAWAKOSEI sheria hizo kwa watu walio ndani ya chama tawala?

Kama haridhiki anachukua hatua gani?

Unadhani kuna utashi wa kisiasa kwa watawala kuona kuwa jeshi la polisi linarekebisha haya wanayokiuka?
 
Pinda anazijua sana sheria sema tu ameamua kujivika uzuzu kwa ajili ya kukitetea chama chake kinachokufa.
Na hili tutaendelea kuwaonesha watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii, kuwa tunapelekwa pabaya na CCM iliyozeeka na kuchoka.
 
Polisi iko hapa ilipo kwa sababu ya elimu duni, ukosefu wa mafunzo yanayoenda na wakati na pia upungufu wa vitendea kazi.

Polisi wengi bado wanaishi kwenye zama za uongozi wa kiimla, na ikichukuliwa kuwa wengi wao wako kwenye nafasi walizozipata kwa sababu polisi ilikuwa na inaendelea kuwa ni sehemu ambayo vijana wengi wanakimbilia baada ya elimu ya juu kuwashinda (form four and six failure), huku wengi wao ndani ya jeshi wakiwa wamegushi vyeti. Hata hao ambao wana vyeti vya juu kama stashahada (degree) basi zinakuwa pasi zake niza chini kabisa au hazina wigo mpana wa ajira nchini.

Polisi hawajazinduka na kupata ufahamu kuwa nchi kwa sasa inaendeshwa na utawala wa sheria ambapo wananchi wake wengi kwa sasa wanafahamu haki na wajibu wao katika nchi.

Tanzania ya sasa, It's not just about law, what's matter now is a technical aspect of law. Hata kesi nyingi kwa sasa nchini zinachambuliwa na kunyambulishwa kwa njia hii.

Polisi ni taasisi ambayo utendaji wake wa kila siku siyo kwamba tu unatakiwa uendane na sheria bali pia lazima wafahamu jinsi ya kuruka viunzi vya sheria technically. Siamini kama mwenye vyeti vya kughushi, form four au form six failure anaweza kuruka viunzi kama hivi kwa sasa.

Polisi ya Tanzania inahitaji OVERHAUL ili kupambana na challenge za karne ya 21 ambazo ni pamoja na kujua sheria na viunzi vya sheria technically.
Mkuu, mjadala wa hapa ulikuwa bado unakuhitaji. Naona kuna maswali uliulizwa hapo juu, tusaidie mawazo yako.
 
1. Utangulizi
Jeshi la Polisi ni chombo cha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichoundwa ili kuwahakikishia wananchi usalama wao na mali zao, kudumisha amani na utulivu katika jamii, pia kuzuia, kubaini na kupambana na uhalifu.

2. Lengo la Jeshi la Polisi:
Jeshi la Polisi lipo kwa lengo la kuwahakikishia wananchi usalama wao na mali zao, kudumisha amani na utulivu katika jamii, pia kuzuia, kubaini na kupambana na uhalifu. Jeshi la Polisi lipo kama sheria inavyoelekeza kuhakikisha kuwa kila mtu, wakiwemo askari polisi wanafuata sheria katika kila hatua.

3. Majukumu ya Jeshi la Polisi:
Jeshi la polisi lina kazi kadhaa:

  1. Kuzuia na kudhibiti uhalifu.
  2. Kubaini na kuchunguza vizuri wakati wowote uhalifu unapotokea.
  3. Kutayarisha shauri la kweli na lenye ushahidi ili mwendesha mashtaka aweze kuwasiliana mahakamani.
  4. Kukusanya taarifa kuhusu matukio katika jamii ili kuweza kutimiza jukumu la kudumisha sheria na utilivu.

4 Sheria inayoongoza shuguli za Jeshi la Polisi:
Shughuli za jeshi la polisi zinaongozwa na sheria mbalimbali, lakini kwa kiasi kikubwa:

  1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.
  2. Sheria ya Jeshi la Polisi namba 322 (Police and Auxiliary Services Act 2002 Cap 322).
  3. Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.
  4. Kanuni za Polisi (Police General orders).
​
Kwa hiyo Jeshi la polisi lina mamlaka ya kisheria na linapaswa kutumia mamlaka hayo kulingana na taratibu zilizoainishwa katika sheria husika.

Polisi wanaweza kukamata, kufanya upekuzi, kushikilia, kumpeleleza mtuhumiwa, kumhoji shahidi, kufanya mahojiano na mtuhumiwa, kutawanya waandamanaji wenye nia ovu na kuhakikisha usalama wa jamii. Wanapaswa kufanya hivyo kwa kufuata taratibu na sheria na sio vinginevyo. Polisi hawawezi kufanya wapendavyo.
Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai inaeleza njia ambazo polisi na mahakama wanapaswa kufuata katika kuwashughulikia wahalifu. Hii ni pamoja na mamlaka ya polisi na taratibu wanazotakiwa polisi wazifuate. Mfano mmojawapo ni matumizi ya nguvu ya polisi pale anapomkamata mtuhumiwa na nguvu za polisi anapofanya uchunguzi
Sheria ya ushahidi inaeleza kwa undani kinachokubalika mahakamani kama ushahidi. Ushahidi wowote uliopatikana kwa kutumia nguvu, hauwezi kutumika kama ushahidi halali, ikibainika mahakamani kuwa ulipatikana kwa njia batili.
Sheria ya Polisi inaeleza kuhusu uendeshaji wake, nidhamu mamlaka na kazi za polisi na mambo mengine yanayolihusu jeshi la polisi. Sheria hii inasisitiza polisi kutenda haki katika utendaji wao ili kutoa mfano wa kulinda sheria na kanuni za nchi.

Matumizi yoyote mabaya ya mamlaka au uzembe katika kazi ni utovu wa nidhamu na uhalifu. Afisa wa polisi anayetenda hayo anapaswa kuchukuliwa hatua stahiki.

5. Gharama za Shughuli za Polisi
Shuguli zote za polisi zinalipwa na walipa kodi wa Tanzania.

Kila mwaka katika kikao cha bajeti, hutengwa fungu maalum kwa ajili ya uwezeshaji wa utoaji wa huduma za polisi katika jamii. Fedha hizi hupitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa jukumu la ulinzi na usalama wa raia ni suala la muungano. Kitengo cha mipango cha jeshi la polisi huandaa mapendekezo ya bajeti, ambayo hupelekwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi kwa ajili ya kuridhia, kasha hupelekwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi tayari kwa kupelekwa bungeni. Wabunge hujadili na kupitisha bajeti ya polisi. Sehemu kubwa ya bajeti huenda kwenye mishahara. Matumizi mengine ni mafunzo, upelelezi, miundombinu, ujenzi na ukarabati wa nyumba n.k.

Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali hufanya ukaguzi wa akaunti na fedha zilizotumiwa na jeshi la polisi kila mwaka, na taarifa za ukaguzi huwasilishwa bungeni

6. Askari Polisi yuko juu ya sheria?
Hakuna mtu aliye juu ya sheria. Watanzania wote wakubwa kwa wadogo, tajiri kwa maskini, wanaume kwa wanawake, bila kujali dini na itikadi, hata wafanyakazi wa serikali na polisi wanatakiwa kutii sheria na kuishi kwa mujibu wa sheria zilizowekwa nchini mwetu chini ya Katiba yetu.

Hii ina maana kila tendo linalofanywa na askari polisi lifanywe kulingana na sheria, na iwapo polisi hawatafanya hivyo watawajibika mbele ya sheria. Matarajio ni kuwa pia sheria zilizotungwa zimezingatia haki na usawa.

Askari anayevunja sheira anapaswa kuadhibiwa. Tena kwa kuwa polisi amepewa dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sheria, adhabu yake inatakiwa iwe kali zaidi anapovunja sheria.

Iwapo askari ametenda kosa la jinai anapelekwa mahakamani na kuhukumiwa kama mtu mwingine. Lakini anaweza kupelekwa mahakama

7. Polisi na Rushwa:
Jina zuri la Jeshi la polisi na sifa njema ya watumishi wake inategemea sana uadilifu na uaminifu wa kila askari polisi. Kila tendo la rushwa au tuhuma za rushwa dhidi ya askari polisi inatoa sifa mbaya kwa jeshi la polisi. Hivyo, kila polisi anayefahamu kuwa polisi mwenzake anajihusisha na vitendo vya rushwa na akashidwa kuchukua hatua yoyoyte atakuwa anafanya makosa na atahusishwa kushiriki.

8. Polisi na Maandamano na Mikutano ya hadhara:
Mtanzania yoyote ana haki ya kushiriki katika maandamano kwa mujibu wa Ibara ya 20 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ibara hii inatoa haki kwa kila mtanzania kushiriki katika mikusanyiko/maandamano ya amani.

Hata hivyo kundi linalofanya mkusanyiko/maandamano hayo katika maeneo ya wazi linapaswa kutoa taarifa kwa polisi si chini ya saa 48 kabla ya mkusanyiko/maandamano hayo. Taarifa inatolewa kwa kiongozi wa polisi wa eneo ambalo mkusanyiko unapendekezwa kufanyika.

Iwapo kiongozi wa polisi anayepokea taarifa hiyo ana sababu ya msingi ya kuona kuwa mkutano unaopendekezwa unaweza kusababisha uvunjifu wa amani na usalama wa umma anaweza kuzuia mkutano huo kufanyika.

Kwa upande mmoja askari polisi wana wajibu wa kuhakikisha amani inakuwepo. Kwa upande mwingine wanapaswa kuwawezesha wananchi kutumia haki yao ya msingi ya kufanya mikutano ya hadhara kwa amani na utulivu.

Matumizi ya Nguvu dhidi ya Maandamano au Mkutano wa hadhara.
Polisi hawapo kwa ajili ya kuwaadhibu watu, bali kwa ajili ya kuhakikisha kuwa watu wapo salama na sheria hazivunjwi.

Inapotokea kuwa polisi wanalazimika kudhibiti mkusanyiko wa watu, wanapaswa wahakikishe kuwa kila wakifanyacho wanatumia kiasi. Watalazimika kutumia nguvu kama suluhisho la mwisho baada ya hatua nyingine zote kushindikana. Hata hivyo, iwapo nguvu italazimika kutumika basi iwe ya kadiri na inayoendana na mazingira, na itumike kwa muda mfupi iwezekanavyo.

9. Matumizi ya Silaha za Moto dhidi ya Raia.
Kama ilivyosemwa hapo juu, polisi watatumia nguvu kubwa pale ambapo imelazimika tu, na ambapo njia nyingine zote za udhibiti zimejaribiwa na kushindikana.

Polisi anaweza kutumia bunduki katika mazingira yafuatayo:

  1. Dhidi ya mtu anayetoroka, au
  2. Dhidi ya mtu anayefanya jaribio la kutoroka toka kizuizini au
  3. Dhidi ya mtu anayefanya jaribio la kutoroka asikamatwe
  4. Dhidi ya mtu anayetumia nguvu kumwondoa mtu mwingine kutoka kizuizi halali
  5. Dhidi ya mtu anayetumia nguvu kuzuia ukamatwaji halali wa mtu mwingine.
  6. Dhidi ya kundi linaloharibu mali au kutishia usalama wa raia baada ya kuonya mara tatu

Lakini pale tu askari anapokuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hawezi kuzuia utoro huo kwa njia nyingine ana ametoa onyo kwa mtu huyo kuwa bunduki itatumika iwapo hatatii na mtu huyo hajali onyo lililotolewa. Pia endapo polisi watakuwa na sababu ya kuamini kuwa wao wenyewe wako hatarini kuumizwa vibaya.

Wanapolazimika kutumia bunduki dhidi ya kundi linalofanya uharibifu au kutishia usalama wa raia, risasi zinapaswa kulengwa chini na katika kundi linaloonekana ni tishio, lakini si kwa lengo la kusababisha mauaji bali kuwatawanya. Mara kundi linapoonyesha dalili la kutawanyika askari wanapaswa kusitisha upigaji risasi.

Polisi wanaolazimika kutumia risasi wanawajibika kutolea maelezo kila risasi waliyotumia kwa kuandika taarifa inayowekwa katika kumbukumbu.

Pale itakapothibitika kuwa polisi ametumia nguvu isiyohitajika atachukuliwa hatua za kinidhamu au kufunguliwa mashtaka kwa kosa la jinai.

10. Haki za Watu wanaowekwa Mahabusu.
Askari polisi wanawajibika kuwapeleka mahakamani watu waliowaweka mahabusu ndani ya masaa 24. Hata hivyo kwa watu waliokamatwa kwa kibali, kwa kosa ambalo adhabu yake ni kifo, polisi lazima wakupeleke mahakamani mapema iwezekanavyo.

Askari hawaruhusiwi kupiga, kutisha au kutia hofu mtu aliyewekwa kizuizini, na anayekiuka anaweza kuadhibiwa kwa kosa hilo.

Askari polisi ana haki ya kuhoji walio kizuizini, lakini hawezi kulazimisha mtu yeyote kuongea kitu chochote ambacho mtuhumiwa hana habari nacho, au kitu ambacho mtu hataki kukisema, au kukiri makosa ambayo polisi wanataka akiri.

Ungamo la kosa mbele ya polisi kwa namna yoyote ile halitakubalika mahakamani kama ushahidi.
Wakati jeshi la polisi liko alert na maandamano ya upinzani, yafaa turudi kujikumbusha haya.
 
Mkuu, kwani Amiri Jeshi mkuu hana sauti juu ya mwenendo huo wa jeshi la polisi?

Je Amiri Jeshi Mkuu anaona kama polisi wanakiuka majukumu yao, au anafurahia kuona wanatenda wanayotenda kwa maslahi ya chama chake?

Kwa nini askari polisi HAWAKOSEI sheria hizo kwa watu walio ndani ya chama tawala?

Kama haridhiki anachukua hatua gani?

Unadhani kuna utashi wa kisiasa kwa watawala kuona kuwa jeshi la polisi linarekebisha haya wanayokiuka?

BILA SHAKA JIBU NI'NDIYO',
Kama amiri jeshi mkuu anajua hili unadhani mapolisi wanajiamulia tu???
Hebu achana na polisi kama moja ya viungo katika mwili angalia na viungo vingine kama vipo sawa.anzia hapo.
 
Back
Top Bottom